Mwalimu wa St. Doroth (Tabora) ashtakiwa kwa kumnajisi Mwanafunzi wa Darasa la Pili

Mwalimu wa St. Doroth (Tabora) ashtakiwa kwa kumnajisi Mwanafunzi wa Darasa la Pili

Hivi wizara ya ustawi wa jamii inafanya kazi gani kuzuwia haya maporomoko ya maadili? Maana huu si mmomonyoko tena, ni maporomoko. Au wanangoja matukio wazime moto?

cc: Dkt. Gwajima D.
 
TABORA - MWALIMU Dotto Elias (29) wa Shule ya mchepuo wa Kiingeza ya Mtakatifu Doroth iliyopo maeneo ya kidatu Manispaa ya Tabora anayedaiwa kumnajisi mwanafunzi wa darasa la pili chooni amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Tabora.

Akisoma mashtaka hayo jana Agosti 15, 2024, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, Charles Magonza aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, John Mdoe kuwa mtuhumiwa alikuwa akimnajisi mtoto huyo (jina limehifadhiwa) chooni kipindi cha kunywa uji.

Alidai Julai 26, 2024 kati ya saa 1 na saa 2 usiku bibi wa mtoto huyo alibaini mtoto huyo kufanyiwa vitendo vya unajisi baada ya kumkagua na kuona alivyoharibiwa.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya Mwaka 2022 Kifungu cha 154 Sura Ndogo ya 15 ya Makosa ya Utu, mtu atakayemwingilia mwenzake kinyume cha maumbile kwa lazima ama kwa kutaka mwenyewe adhabu yake/zao wote ni kifungo cha maisha gerezani au kifungo cha miaka 30 jela.

Mshtakiwa Elias baada ya kusomewa mashitaka yake alikana kutenda kosa hilo kwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka saba.

Chanzo: Habari Leo
hawa ummbwa wangekua wanahasiwa ingependeza sana
 
hawa ummbwa wangekua wanahasiwa ingependeza sana
No one shall be condemned unheard.

Usimhukumu kabla ya kumsikiliza kwanza. Dunia ya Sasa Ina mambo mengi Sana. Kuna suala la visasi, chuki binafsi, wivu, kugombea vyeo makazini, n.k, n.k,
Huko maofisini na makazini Watu wapo kwenye Vita kali Sana ya kugombea madaraka au vyeo. Usione ukadhani! Kuwa mtulivu sana kwenye masuala kama haya.
 
Mkuu wa Mkoa kamwambia mzazi mwenye majonzi "haya yatakwisha." Mtoto ambae kaachiwa kovu la maisha physically na psychologically

Halafu kaamuru mwananchi anaewashawishi familia wakae chini wayamalize akamatwe na polisi! Sijui kwa kesi gani

Na sielewi kwa nini wilayani na mkoani huwa hakuna mwendesha mashtaka aliyesomea sheria, na mwenye mamlaka ya kufungua kesi ya jinai, kuwatua mzigo hawa "wenyeviti wa ulinzi na usalama" ambao kwenye sheria ni ma dunderhead
Dunderhead
 
Vijana acheni kula 0. Unaanza taratibu kula wanawake mwisho unakula na watoto
 
Binadam wa sasa ni wa kuogopa mno, bila kujali uko nae karibu kiasi gani..husiana na biandamu mwenzio kwa tahadhari za juu sana iwe ni kibiashara, kiimani na kokote kule..kaa macho sana
 
TABORA - MWALIMU Dotto Elias (29) wa Shule ya mchepuo wa Kiingeza ya Mtakatifu Doroth iliyopo maeneo ya kidatu Manispaa ya Tabora anayedaiwa kumnajisi mwanafunzi wa darasa la pili chooni amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Tabora.

Akisoma mashtaka hayo jana Agosti 15, 2024, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, Charles Magonza aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, John Mdoe kuwa mtuhumiwa alikuwa akimnajisi mtoto huyo (jina limehifadhiwa) chooni kipindi cha kunywa uji.

Soma Pia: Mwalimu Mkuu adaiwa kumlawiti mwanafunzi Bunda

Alidai Julai 26, 2024 kati ya saa 1 na saa 2 usiku bibi wa mtoto huyo alibaini mtoto huyo kufanyiwa vitendo vya unajisi baada ya kumkagua na kuona alivyoharibiwa.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya Mwaka 2022 Kifungu cha 154 Sura Ndogo ya 15 ya Makosa ya Utu, mtu atakayemwingilia mwenzake kinyume cha maumbile kwa lazima ama kwa kutaka mwenyewe adhabu yake/zao wote ni kifungo cha maisha gerezani au kifungo cha miaka 30 jela.

Mshtakiwa Elias baada ya kusomewa mashitaka yake alikana kutenda kosa hilo kwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka saba.

Chanzo: Habari Leo
Tunapoambiwa kuwa mwisho wa Dunia umefika mwisho wake tuelewe, haya matukio yamekithiri san. TUTUBUNI DHAMBI ZETU kwani YESU Yu karibu anabisha .

Shetani anaweza kumtumia mtu kufanya ukatili wa aina yoyote na sisi tukaona ni madhaifu ya mtu kumbe ni HAPANA si yeye. TUOMBEANA WATANZANIA hali mbaya inakuja.

I love jamiiforums
 
Tatizo kwenye shule za private wanafunzi ni wachache mno so ni rahisi kwa mwalimu kumlawiti mwanafunzi chooni. Mabinti wengi wanao soma shule za private huwa wanavunjwa bikira wakiwa darasa la 6 au la7 na huwa wanavunjiwa chooni... kwa sababu mazingira yanaruhusu.

Jambo hilo ni gumu sana kufanyika Kayumba kwa sababu kunakuwa na watoto wengi sana so ni ngumu sana mwalimu kumnajisi mtoto chooni.

Dawa ni kupeleka watoto wenu shule za Kayumba period.

uwingi wa watoto kwenye shule za Kayumba ni ulinzi pia.
 
Back
Top Bottom