Mwalimu wa Tanzania aunganisha tamaduni kupitia lugha ya Kichina na opera ya jadi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
1778698894609950.jpg

Katika chumba cha mihadhara katika Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dodoma nchini Tanzania, Tausi Iddi Nzimano, anayejulikana kwa jina lake la Kichina kama Lin Shi, hubadilisha kati ya lugha ya Kichina na Kiswahili bila shida anapowaongoza wanafunzi kwenye matamshi, sauti, na misemo ya jadi.

Kwake yeye, kujifunza lugha ya Kichina sio tu shughuli ya kitaaluma bali ni njia ambayo imebadilisha kazi yake, utambulisho wake, na mtazamo wake kuhusu ulimwengu.

Nzimano, mhadhiri msaidizi katika Kitivo cha Uhandisi cha chuo kikuu hicho na mwalimu wa lugha ya Kichina katika Taasisi ya Confucius, amefanya kazi katika taasisi hiyo kwa karibu miaka sita. Alianza kufundisha Kichina mwaka 2022, lakini safari yake ya lugha hiyo ilianza mapema zaidi, akiwa shule ya sekondari.

"Siku zote nimekuwa nikipenda lugha," alisema. "Kabla ya Kichina, nilisoma Kiswahili, Kiingereza, na Kifaransa. Nilipowaona walimu wa Kichina kwa mara ya kwanza wakifundisha katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Zanaki jijini Dar es Salaam, nilidhani hii ilikuwa nafasi yangu ya kujifunza lugha mpya.”

Miaka ya mwanzo ilikuwa na changamoto. Kutokana na fursa chache za kufanya mazoezi ya kuzungumza nje ya darasa, aliamua kujifunza mwenyewe nyumbani, kutazama filamu za Kichina, kusikiliza muziki, na kuimba nyimbo za Kichina ili kuboresha ufasaha wake.

"Wakati huo, watu wachache sana walikuwa wakijifunza Kichina," alisema. "Sasa wanafunzi wengi wanakisoma kwa sababu wanakiona kama somo linalofungua milango ya kazi na ajira."

Jitihada zake hatimaye zilimpeleka China, ambapo alikaa mwaka mmoja akisoma isimu katika Chuo Kikuu cha Anga cha Zhengzhou. Ni kipindi hiki ndipo ambapo alijionea kwa mara ya kwanza opera ya jadi ya Kichina, wakati ambao uliacha hisia ya kudumu.

Zheng Xueyu, mkurugenzi wa Kichina wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dodoma, alimpangia asafiri kwenda mji wa Luoyang kusoma Yuju, aina ya opera ya jadi ambayo ilitokea katika Mkoa wa Henan, China.

"Nilipoona onyesho hilo kwa mara ya kwanza, nilishangaa," alikumbuka. "Uimbaji ulikuwa na nguvu na wa kisanii."

Akitiwa moyo na shauku yake ya kuimba, aliamua kukabili changamoto ya kujifunza aina hiyo ya sanaa. Yuju inajulikana kwa uwasilishaji wake mzuri wa sauti, usemi wazi, na melodi zenye mdundo, na ni mojawapo ya mila maarufu zaidi za opera katika mkoa huo nchini China.

Kwa Nzimano, kuijua ilikuwa jambo gumu na lenye faida. Mavazi, vipodozi, ishara, na mbinu za sauti zilihitaji nidhamu na jitihada, lakini pia ziliongeza upendo wake wa utamaduni wa Kichina.

"Kila kitu kilivutia kuhusu opera hiyo," alisema. "Hata baadhi ya Wachina waliniambia wao pia hawawezi kujifunza kwa urahisi, kwa hivyo walishangaa kuniona naweza kuifanya kwa muda mfupi."

Uzoefu wake nchini China, ulibadilisha mwelekeo wa maisha yake.

"Kujifunza Kichina kulinifanya nipate kazi. Bila ya Kichina, nisingekuwa na kazi niliyonayo leo," alisema. "Pia ilinipa fursa ya kusoma nje ya nchi na kupata uzoefu wa ulimwengu tofauti. Sasa najiona kama daraja kati ya Tanzania na China."

Hadithi yake inaonesha mwelekeo mpana katika Taasisi ya Confucius, ambapo idadi inayoongezeka ya wanafunzi wa Tanzania wanakubali masomo ya lugha ya Kichina kwa ajili ya kuelewa utamaduni na fursa za ajira.

Miongoni mwao ni Loyce Johansen Mashurubu mwenye umri wa miaka 22, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa lugha ya Kichina anayejulikana kwa jina lake la Kichina kama Li Yue.

"Nilichagua kozi hii kwa sababu kujifunza Kichina kunavutia sana," alisema. "Pia nataka kusoma nje ya nchi nchini China."

Kupitia masomo yake, Mashurubu amepata uzoefu sio tu wa lugha hiyo bali pia wa utamaduni, sikukuu, na vyakula vya Kichina.

"Sasa najua kuhusu Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, Sikukuu ya Mwezi, na Sikukuu ya Mashua ya Dragon," alisema. "Pia nimejifunza kuhusu vyakula kama vile jiaozi na baozi. Inafurahisha sana."

"Kuna watu na makampuni mengi zaidi ya Kichina katika nchi yetu," alisema. "Kujifunza Kichina hutoa fursa nyingi, hasa kwa ajira. Katika siku zijazo, tutakuwa watafsiri bora."

Nyuma ya shauku inayokua ya wanafunzi kuna juhudi za kitaasisi zilizopangwa zinazoongozwa na Taasisi ya Confucius na walimu wake wa Wachina na Watanzania.

Mwalimu wa Kichina Zheng Xueyu amekuwa akijishughulisha na elimu ya Kichina nchini Tanzania tangu 2013. Ametumikia majukumu mengi, ikiwa ni pamoja na kusimamia programu za lugha za sekondari, na akarudi mwaka 2024 kuendelea kuongoza taasisi hiyo.

Kwa sasa, taasisi hiyo inatoa programu za shahada ya kwanza za lugha ya Kichina ikiwa na wanafunzi karibu 350 waliojiandikisha. Pia ina walimu 14 wazawa, 11 katika Chuo Kikuu cha Dodoma na watatu katika darasa la satelaiti katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro.

"Tunazingatia zaidi kuwafunza walimu wazawa," Zheng alisema. "Kila mwaka tunatoa mafunzo katika upangaji wa masomo, muundo wa darasa, mbinu za kufundisha, na usimamizi wa darasa. Pia tunawaongoza walimu kuelewa utamaduni na adabu za Kichina."

Alimtaja Nzimano kama mfano wa mafanikio ya ujenzi wa uwezo na mawasiliano ya kitamaduni. Baada ya kuhitimu kwenye taasisi hiyo, alijiunga akiwa mwalimu mwenyeji na baadaye akashiriki katika mafunzo ya ngazi ya juu nchini China, ikiwa ni pamoja na kujifunza sanaa za jadi za opera.

"Nzimano alionesha kupendezwa sana na utamaduni wa jadi wa Kichina na sanaa za maonesho," alisema. "Baada ya kupata mafunzo zaidi huko Luoyang, alifanya vizuri sana na hata aliimba kwenye mahafali ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Anga cha Zhengzhou, ambayo iliwavutia watu wengi."

Mkazo muhimu, Zheng aliongeza, ni kuunganisha kujifunza lugha ya Kichina na ufundi stadi ili kukidhi mahitaji makubwa ya soko la ajira.

Kwa mujibu wa Zheng, programu ya shahada ya kwanza ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Dodoma inaendelea kuwa ya aina yake nay a kipekee nchini Tanzania. Wahitimu wanazidi kuhitajika, hasa kwenye makampuni ya Kichina yanayofanya kazi nchini.

"Hadi wanapofikia mwaka wao wa tatu, wanafunzi wengi wanakuwa tayari wameajiriwa," alisema. "Wengi hawahudhurii maonesho ya ajira kwa sababu tayari wana fursa za ajira au wanapanga kuendelea na masomo nje ya nchi."

Kwa walimu na wanafunzi, athari ya elimu ya lugha ya Kichina inavuka nje ya madarasa na ajira, inakuza uelewa wa utamaduni na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China.

Kama Nzimano anavyosema: "Lugha ya Kichina imebadilisha maisha yangu. Imenipa fursa, uzoefu, na utambulisho mpya. Sasa ninawasaidia wengine kugundua njia hiyo hiyo."
 
View attachment 3629963

Safi kabisa Kuna mwanangu anasoma hapo, kichina!_UDOM.
 
Back
Top Bottom