Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Katika utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Mwalimu Yusuph Ibrahim mwenye ulemavu wa mguu leo Oktoba 13, 2025, amekabidhiwa mguu wa bandia wenye thamani ya Tsh Milioni 46 kama utekelezwaji wa ahadi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuguswa na moyo, ari ya mwalimu huyo katika ufundishaji wake.
Akikabidhiwa mguu huo katika Ofisi ya Afisa Uhusiano Taasisi ya Mifupa MOI Muhimbili Dar es Salaam, Mwalimu Yusuph ametoa shukrani zake kwa Rais Samia Suluhu akieleza mguu huo utakuwa chachu katika kuongeza ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku kama mwalimu mwenye jukumu la kuliandaa taifa la kesho.