Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Emmaus Mwamakula amesema anatafakari na kuweka mkakati upya ulioboreshwa zaidi kisha atautangaza kwa Watanzania.
Februari 15, 2021. Mwamakula alikamatwa na polisi kwa madai ya kuhamasisha maandamano ya kudai tume huru na Katiba Mpya kwa njia ya mtandao lakini alikamatwa na kuwekwa rumande kwa siku moja.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano Februari 17, 2021 nyumbani kwake Kimara jijini Dar es Salaam amesema mwishoni mwaka 2020 aliutangazia umma kusudio lake la kuongoza matembezi ya hiari nchi nzima lengo likiwa kuhamasisha upatikanaji wa Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi.
Amebainisha kuwa azma ya kuongoza matembezi hayo ilichangiwa na sababu kadhaa ikiwemo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 baada ya kuzunguka nchi nzima na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu.
“Nilizunguka bara na visiwani pamoja na mambo mengine nilijionea na kushuhudia jinsi mchakato mzima wa uchaguzi ulivyoathiriwa na vitendo vya ukiukwaji na upendeleo wa wazi.”
“Vitendo hivyo ni pamoja na kuwaengua kwa kiasi kikubwa wagombea wa vyama vya upinzani katika nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge,” amedai.
Amesema mwanzoni mwa Februari, 2021 alitangaza kuzindua matembezi ya hiari jijini Dar es Salaam kuanzia Februari 16, 2021.
“Nilielekeza wazi kuwa watu watatembea katika makundi ya watu 10 hadi 20 na kwamba kutakuwa na umbali usiopungua mita 100 kati ya kundi na kundi na kwamba matembezi hayo yataelekezwa katika ofisi yoyote ya umma,” alieleza akibainisha kuwa nia yake hiyo ilizimwa baada ya kukamatwa na kupelekwa kituo cha polisi Oysterbay.
Amesema licha ya kutofanikiwa kuandaa matembezi hayo lakini kuzuiwa kwake kumesaidia uzinduzi wa kampeni zenyewe.
Chanzo: Mwananchi