Mwamakula: Naweka mkakati upya ulioboreshwa zaidi kisha nitautangaza kwa Watanzania

Mwamakula: Naweka mkakati upya ulioboreshwa zaidi kisha nitautangaza kwa Watanzania

Ndio nimeuliza kuna ulazima wa hilo la kufanya matembezi kudai katiba katika hali tuliyopo ambapo watu wanakufa na matatizo ya kushindwa kupumua na tunazika watu kila siku?
Hali iliyopo chukua hatua wewe binafsi.
 
Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Emmaus Mwamakula amesema anatafakari na kuweka mkakati upya ulioboreshwa zaidi kisha atautangaza kwa Watanzania.

Februari 15, 2021. Mwamakula alikamatwa na polisi kwa madai ya kuhamasisha maandamano ya kudai tume huru na Katiba Mpya kwa njia ya mtandao lakini alikamatwa na kuwekwa rumande kwa siku moja.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano Februari 17, 2021 nyumbani kwake Kimara jijini Dar es Salaam amesema mwishoni mwaka 2020 aliutangazia umma kusudio lake la kuongoza matembezi ya hiari nchi nzima lengo likiwa kuhamasisha upatikanaji wa Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi.

Amebainisha kuwa azma ya kuongoza matembezi hayo ilichangiwa na sababu kadhaa ikiwemo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 baada ya kuzunguka nchi nzima na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu.

“Nilizunguka bara na visiwani pamoja na mambo mengine nilijionea na kushuhudia jinsi mchakato mzima wa uchaguzi ulivyoathiriwa na vitendo vya ukiukwaji na upendeleo wa wazi.”

“Vitendo hivyo ni pamoja na kuwaengua kwa kiasi kikubwa wagombea wa vyama vya upinzani katika nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge,” amedai.

Amesema mwanzoni mwa Februari, 2021 alitangaza kuzindua matembezi ya hiari jijini Dar es Salaam kuanzia Februari 16, 2021.

“Nilielekeza wazi kuwa watu watatembea katika makundi ya watu 10 hadi 20 na kwamba kutakuwa na umbali usiopungua mita 100 kati ya kundi na kundi na kwamba matembezi hayo yataelekezwa katika ofisi yoyote ya umma,” alieleza akibainisha kuwa nia yake hiyo ilizimwa baada ya kukamatwa na kupelekwa kituo cha polisi Oysterbay.

Amesema licha ya kutofanikiwa kuandaa matembezi hayo lakini kuzuiwa kwake kumesaidia uzinduzi wa kampeni zenyewe.

Chanzo: Mwananchi
Aangalie asijepotezwa na wasiojulikana
 
Hali iliyopo chukua hatua wewe binafsi.
Kuchukua hatua ni pamoja na kuepuka na misongamano isiyo ya lazima,sasa hiyo katiba imeanza kulalamikiwa leo?iweje huyo Askofu atake kuwakusanya watu kudai katiba katika kipindi ambacho watu wanajitahidi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima? huoni kama anarudisha nyuma jitihada za watu kujikinga na corona?
 
Mbona kaeleza jinsi atakavyoepuka misongamano kwenye maelezo yake. Tafuta muda usikilize speech zake
 
Mbona kaeleza jinsi atakavyoepuka misongamano kwenye maelezo yake. Tafuta muda usikilize speech zake
Kuna ulazima huo wa kufanya hayo matembezi wakati huu ambako kuna hatari ya maambukizi ya corona?wakati watu kipindi hiki wanajaribu kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima yeye ndio kaona kipindi ndio cha kuwatembeza watu kwa makundi kwa ulazima gani ni kipi hicho kinachomfanya aone ni lazima afanye sasa?
 
Kumbe ni matembezi na sio maandamano!.
Ndio maana aliwashinda waliomnukuu vibaya.
 
Kuna ulazima huo wa kufanya hayo matembezi wakati huu ambako kuna hatari ya maambukizi ya corona?wakati watu kipindi hiki wanajaribu kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima yeye ndio kaona kipindi ndio cha kuwatembeza watu kwa makundi kwa ulazima gani ni kipi hicho kinachomfanya aone ni lazima afanye sasa?

Corona haizuii matembezi ya hiari... Raia watachukua tahadhari zote na kudumisha amani...
 
Corona haizuii matembezi ya hiari... Raia watachukua tahadhari zote na kudumisha amani...
Watu gani wa kuchukua tahadhari?hivi wewe umeona kwenye huo msiba wa leo jinsi watu walivyokusanyana tena bila barakoa,watu kama hao ndio wa kuchukua tahadhari? Ndio maana nauliza kuna ulazima hasa wa kufanya hayo matembezi wakati huu?
 
Tungekuwa na Maaskofu walau 10 tu kama huyu Mwamakula, hakika Taifa letu lisingetawaliwa na duhuluma, ubabe, ukatili, ubinafsi, uonevu, ukabila na kila aina ya madudu.

Hongera sana Askofu Mwamakula. Mamilioni ya Watanzania wapenda Mabadiliko ya kweli, tuko nyuma yako.

Yupo Askofu Dr. Josephàt Gwajima. Yeye unamweka kundi gani kwani?
 
Kichwa kinajielewa sana hiki, naona furaha mno kuona watu wasio na unafiki ndani mwao.
 
Back
Top Bottom