DOKEZO Mwamba ajenga fremu kituo cha Mwendokasi Mbagala licha ya kupigwa stop na serikali

DOKEZO Mwamba ajenga fremu kituo cha Mwendokasi Mbagala licha ya kupigwa stop na serikali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
IMG_20240105_141647.jpg
IMG_20240106_084848.jpg

Bila shaka huyu ni kigogo mzito sana, anajenga frem kwenye hifadhi ya barabara, ndani ya kituo cha mwendokasi Mbagala, kibali amepata wapi? Ilikuja Tanroad ikasimamisha ujenzi na kupiga X jamaa akafuta kwenye x za kijivu ujenzi unaendelea, wakaja tena wakarudia kupiga X bado mafundi wanapaua kwwa kasi. Idadi ya frem ni nyingi sana.

Ni nani huyu ambaye ni mkubwa kuliko serikali?
Mkuu wa mkoa amemshindwa?
Meneja wa Tanroad amemshindwa?
Dar wamemshindwa?
Wizara ya ardhi imemshindwa?
Je Jery Silaa anajua hii?
Nikitazama najisemea hakuna kikubwa duniani kama pesa na madaraka. Utafanya unavyotaka.

Madhara ya ujenzi huu yatakuwa makubwa sana sababu zitabinya upana wa barabara kwa magari na wateja wanaofanya manunuzi, hivyo kuongeza kero nyingine kwa watumiaji.

TAKUKURU yachukua hatua ~ TAKUKURU yasema UDART walisaini makubaliano batili kujenga maduka katikati ya Barabara
 
Rushwa tu inatembea,ukija na vi X vyako unatiwa pesa unatuli mana sa100 karuhusu.
 
View attachment 2863230View attachment 2863234
Bila shaka huyu ni kigogo mzito sana, anajenga frem kwenye hifadhi ya barabara, ndani ya kituo cha mwendokasi Mbagala, kibali amepata wapi? Ilikuja Tanroad ikasimamisha ujenzi na kupiga X jamaa akafuta kwenye x za kijivu ujenzi unaendelea, wakaja tena wakarudia kupiga X bado mafundi wanapaua kwwa kasi. Idadi ya frem ni nyingi sana.

Ni nani huyu ambaye ni mkubwa kuliko serikali?
Mkuu wa mkoa amemshindwa?
Meneja wa Tanroad amemshindwa?
Dar wamemshindwa?
Wizara ya ardhi imemshindwa?
Je Jery Silaa anajua hii?
Nikitazama najisemea hakuna kikubwa duniani kama pesa na madaraka. Utafanya unavyotaka.

Madhara ya ujenzi huu yatakuwa makubwa sana sababu zitabinya upana wa barabara kwa magari na wateja wanaofanya manunuzi, hivyo kuongeza kero nyingine kwa watumiaji.
Kumbe Serikali ni kubwa au iko juu ya wananchi? Ndio maana WaTz tunabinywa kwa kuwa na mtazamo kama huu.
Serikali ni ya wananchi, kwa ajili ya wananchi ambao ndio wenye nchi na wenye Serikali. Sio lazima mhusika awe mkubwa kuliko Serikali, bali makubaliano kati yake na serikali yake.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Huyo atakuwa kigogo tu
Wanajuana wenyewe
Hapo wangekuwa machinga ,wadada poa wangeondolewa faster

Ova
 
Back
Top Bottom