DOKEZO Mwamba ajenga fremu kituo cha Mwendokasi Mbagala licha ya kupigwa stop na serikali

DOKEZO Mwamba ajenga fremu kituo cha Mwendokasi Mbagala licha ya kupigwa stop na serikali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwani mamlaka gani inayomzuia Hugo mwamba anaefanya jambo jema la kujenga frem
 
Huwezi tenganisha frem/ soko / machinga na frem labda kama unakaa masaki ndo huwezi ona ni ajira ngapi utazalisha kupitia frem hizo.
 
Ubunifu wa hali ya juu kabisa,anataka abiria mkiwa kwenye mwendokasi unatoa mkono nje unanunua unachotaka unaokoa muda,safi kabisa watu kama hawa ndo tunawataka.
 
Hata stand ya nwendo Kasi gerezani ilitakiwa izungukwe na mafrem ili kupunguza tatizo la ajira na jiji kuingiza si chini ya billion tatu kwa mwezi
 
View attachment 2863230View attachment 2863234
Bila shaka huyu ni kigogo mzito sana, anajenga frem kwenye hifadhi ya barabara, ndani ya kituo cha mwendokasi Mbagala, kibali amepata wapi? Ilikuja Tanroad ikasimamisha ujenzi na kupiga X jamaa akafuta kwenye x za kijivu ujenzi unaendelea, wakaja tena wakarudia kupiga X bado mafundi wanapaua kwwa kasi. Idadi ya frem ni nyingi sana.

Ni nani huyu ambaye ni mkubwa kuliko serikali?
Mkuu wa mkoa amemshindwa?
Meneja wa Tanroad amemshindwa?
Dar wamemshindwa?
Wizara ya ardhi imemshindwa?
Je Jery Silaa anajua hii?
Nikitazama najisemea hakuna kikubwa duniani kama pesa na madaraka. Utafanya unavyotaka.

Madhara ya ujenzi huu yatakuwa makubwa sana sababu zitabinya upana wa barabara kwa magari na wateja wanaofanya manunuzi, hivyo kuongeza kero nyingine kwa watumiaji.
Muulizeni mkuu wa mkoa japo atawafokea msisikilize jibu lake hata hivyo fremu zote tayari zimeuzwa, Mbagala kuna vituko!
 
Muulizeni mkuu wa mkoa japo atawafokea msisikilize jibu lake hata hivyo fremu zote tayari zimeuzwa, Mbagala kuna vituko!
Mkuu wa mkoa sahv yuko bize na kutaka kuivunja ddc kariako wajenge jengo wenyewe wanasema la kisasa lenye frame 400 [emoji1]

Ova
 
Back
Top Bottom