Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
Kutana na Mdukuaji Rui Pinto, aliyewaweka Manchester City matatizoni baada ya kudukua barua pepe za Man City mwaka 2015 akiwa nchini kwao Ureno na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari na kuibua uchunguzi dhidi ya City.
Licha ya kusifiwa na sehemu kubwa ya Ulimwengu wa Soka, Pinto alikamatwa na vyombo vya dola, Pinto yupo jela na akabiliwa na makosa 90 ya udukuaji, kuhujumu na udanganyifu.
Taarifa za UEFA kuifungia Man City kwa misimu miwili mfululizo imeibua jambo lingine ambalo limeshika taswira mpya ambapo watu wanataka Pinto aachiwe huru, na jana Ijumaa kuliibuka na Hashtag #FreePinto
Pinto aliandika hivi kupitia ukurasa wake wa Twitter: β Ureno wanataka kuninyamazisha na kuficha kile nilichonacho kwenye Laptop yangu, wanaogopa. Na nina uhakika kwamba sitopewa hukumu ya haki huku Ureno.