Mwamba huyu ndiye aliyewachoma Man City

Mwamba huyu ndiye aliyewachoma Man City

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Kutana na Mdukuaji Rui Pinto, aliyewaweka Manchester City matatizoni baada ya kudukua barua pepe za Man City mwaka 2015 akiwa nchini kwao Ureno na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari na kuibua uchunguzi dhidi ya City.

Licha ya kusifiwa na sehemu kubwa ya Ulimwengu wa Soka, Pinto alikamatwa na vyombo vya dola, Pinto yupo jela na akabiliwa na makosa 90 ya udukuaji, kuhujumu na udanganyifu.

Taarifa za UEFA kuifungia Man City kwa misimu miwili mfululizo imeibua jambo lingine ambalo limeshika taswira mpya ambapo watu wanataka Pinto aachiwe huru, na jana Ijumaa kuliibuka na Hashtag #FreePinto

Pinto aliandika hivi kupitia ukurasa wake wa Twitter: “ Ureno wanataka kuninyamazisha na kuficha kile nilichonacho kwenye Laptop yangu, wanaogopa. Na nina uhakika kwamba sitopewa hukumu ya haki huku Ureno.

View attachment 1358337

IMG_20200215_122542.jpeg
IMG_20200215_122538.jpeg
IMG_20200215_122535.jpeg
 
Huyu jamaa sio yule alimmwagia Sepp Blatter mapesa kwenye mkutano?
 
Watupe sisi Tanzania huyo kijana, tunamhitaji sana, ili aje kumsaidia Prof. Assad kwenye kutafuta majibu ya upotevu wa zile Trillion 1.5 zisizojulikana matumizi yake. Atupe majibu zilipokwenda.[emoji848][emoji2955]

Tutamlinda kwa "ALBADIRI" wakati akifanya kazi zake hapa tanzania.
 
Wadukuaji wengi na wataalamu wa Mambo ya IT ulaya uwa wananywele za kuku kishingo!!!
 
Back
Top Bottom