GE2025 Mwambegele: Tumehakikisha wapiga kura wanapata vituo vya karibu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, ametembelea na kujionea maandalizi ya ujenzi wa vituo 83 kati ya 90 vya wapiga kura vilivyotengwa maalum kwa ajili ya wakazi wa maeneo ya zamani ya Kata za Ilangu, Ipwaga, Bulamata na Mishamo, zilizokuwa chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, ambazo zilifutwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287.

Soma pia: Jaji Mwambegele: Kura ya Mapema kwenye Uchaguzi Mkuu 2025 itapigwa Zanzibar pekee

Jaji Mwambegele amefanya ziara hiyo Oktoba 26, 2025, katika Kata ya Tongwe, Kitongoji cha Luhafwe, akiwa ameambatana na Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa wa Katavi, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanganyika na watendaji wengine wa Tume, kwa lengo la kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.

Akizungumza katika eneo la mnada wa Kitongoji cha Luhafwe, Jaji Mwambegele amesema Tume ilitangaza kuhamisha baadhi ya vituo vya kupigia kura vilivyokuwa ndani ya makazi ya wakimbizi, na kwamba amefika kujiridhisha na utekelezaji wa uhamishaji huo. Amesema Tume imeweka matangazo katika maeneo yaliyofutwa na imehakikisha vituo vipya vinapatikana katika maeneo jirani ili kurahisisha upigaji kura.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanganyika, Bi. Kagemlo Mutagwaba, amesema wapiga kura kutoka kata zilizofutwa wamehamasishwa vya kutosha na wameonesha utayari wa kujitokeza kupiga kura katika vituo vipya vilivyotengwa.

Watanzania wanatarajiwa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani tarehe 29 Oktoba, 2025,
 
View attachment 3494416

Takataka
 
Back
Top Bottom