Mwambie mdogo wako anayekwenda Chuo, sisi pia tulienda tukapata degree

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi.

2. Mwambie Kufaulu Taaluma sio Kufaulu maisha.

3. Mwambie Kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi.

4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea Mtwara, tena kule ndanindani.

5. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba.

6. Mwambie semester1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile.

7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni.

8. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki5 ya chuoni sio Laki5 ya nyumbani.

9. Mwambie chuoni atakutana na semina mbalimbali za ujasiriamali ila chaajabu kila mtu anauza ubuyu na kalamu. Ajaribu bahati yake.

10. Mwambie ajiandae kupokea lawama na hata kuachana na yule mpenzi wake aliyemwacha nyumbani.

11. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanajua kila kitu na wako juu ya sheria hivyo kama ni wa kike ajifunze kusali.

12. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.

13. Mwambie kama ni wa kike,marafiki zaidi ya 3 hatoweza kudumu nao. Watagombana tu.

14. Mwambie kwa "Kapuku",kila mtu huwa anataka kuwasaidia wazazi awapo chuoni lakini kuna nyakati inakuwa nje ya uwezo wetu.

15. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima.

16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau.

17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza Connection na watu muhimu.

18. Migomo na mihemuko yenye uhovu aviepuke maana si kila aliyeko chuon amekuja kusoma bali wengine ndo wako kazin

19. Mwambie zile bata alizokuwa akiskia zikibadilika asishangae.

20.Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amewin maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia

21. Mwambie Maisha ni mafupi sana Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote.
 
Nimepitia andiko lako nimekuta umetumia maneno mengi lakini machache yamenivutia zaidi; Kusali,Mungu,Makanisa/Misikiti

Sio lazima, lakini Kwa Kijana anayeenda Chuo akijikita kukumbuka hayo uliyoandika nina imani maisha yake ya Chuo yataenda Vizuri na atahitimu pasi na shida

Binafsi nashukuru malezi niliyopata utotoni yalinijenga sana kuanzia Sunday Schools, Kipaimara na hata maisha ya Sekondari hasa kupitia UKWATA
 
Duhh natamani kweli na mimi nifike chuo kikuu nijionee ila hii akili sidhani kama hata form four hii nitatoboa
 
1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi.

2. Mwambie Kufaulu Taaluma sio Kufaulu maisha.

3. Mwambie Kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi.

4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea Mtwara, tena kule ndanindani.

5. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba.

6. Mwambie semester1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile.

7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni.

8. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki5 ya chuoni sio Laki5 ya nyumbani.

9. Mwambie chuoni atakutana na semina mbalimbali za ujasiriamali ila chaajabu kila mtu anauza ubuyu na kalamu. Ajaribu bahati yake.

10. Mwambie ajiandae kupokea lawama na hata kuachana na yule mpenzi wake aliyemwacha nyumbani.

11. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanajua kila kitu na wako juu ya sheria hivyo kama ni wa kike ajifunze kusali.

12. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.

13. Mwambie kama ni wa kike,marafiki zaidi ya 3 hatoweza kudumu nao. Watagombana tu.

14. Mwambie kwa "Kapuku",kila mtu huwa anataka kuwasaidia wazazi awapo chuoni lakini kuna nyakati inakuwa nje ya uwezo wetu.

15. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima.

16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau.

17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza Connection na watu muhimu.

18. Migomo na mihemuko yenye uhovu aviepuke maana si kila aliyeko chuon amekuja kusoma bali wengine ndo wako kazin

19. Mwambie zile bata alizokuwa akiskia zikibadilika asishangae.

20.Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amewin maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia

21. Mwambie Maisha ni mafupi sana Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote.
Kuna moja imenishika ndipo natamani ningepata darasa hili since first year ila ndo tushamaliza ss tupo kitaa
 
Back
Top Bottom