Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Juzi imetolewa Tuzo ya mhamasishaji bora wa ligi na TFF kwa hiyo wanatambulika rasmi.Kwanza hawa wahamasishaji ni kazi ambayo haiongezi chochote kwani mashabiki wa Simba na Yanga ni watu ambao popote walipo wapo royal kwa timu zao ni kazi ya viongozi kutengeneza timu bora na kusajili vizuri na kuweka benchi la ufundi lenye tija kwani timu ikishinda mashabiki wenyewe watajaa kila mechi na jezi watanunua tu bila kuhamasishwa, huu ujanja ujanja kwenye mpira haufai kwani unatupoteza kama taifa na matokeo yake tunakua na timu ya taifa mbovu kuliko kawaida.