Mwambieni January Makamba kuwa kazi ya Uwaziri siyo lelemama

Mwambieni January Makamba kuwa kazi ya Uwaziri siyo lelemama

KaziIendelee

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2013
Posts
327
Reaction score
229
Nawasalimu sana wanajamvi,

Chondechonde kazi ya Uwaziri sio lelemama na hasa kwa nafasi yake. HUKU mikoani umeme hakuna, nchi ipo gizani lakini yeye yupo busy kugawa mitungi midogo ya gesi badala ya yeye kama Waziri wa Nishati kuangalia mambo yenye "impact" kubwa kwa watanzania kama suala la kukatikakatika kwa umeme.

Kama kuna mgao wa umeme Watanzania waelezwe. Sisemi haifai wewe kugawa Taifa na Orxy gas huko ila hilo hata Orxy au Taifa wangefanya kwa kushirikiana na wasaidizi wako kwa niaba ya Wizara.

Watu wakisema unaanza kusema unasemwa, HAPANA.

Fanya kazi, kuna shida mahala.
 
Makamba kapita picha na Dkt Kalemani ili kusafisha nyota ila bado sana. Mpaka siku atubu kushiriki
 
Makamba na Mitungi!!
Siasa nimenyanyua 🙌🙌
 
Makamba kapita picha na Dkt Kalemani ili kusafisha nyota ila bado sana. Mpaka siku atubu kushiriki
Anazingua sana....,amefanya kazi na jpm kuna jambo la kujifunza pamoja na madhaifu ya kila mmoja wetu. Katika utumishi ukizidisha uongozi ukaacha nyuma utawala unakuwa wa hovyo na kinyume chake ni sawa.
 
Mi namwambia tu hiyo aina ya uendeshaji misafara yake barabarani yakitokea yakutokea,Mungu asihusishwe!
 
Mnautaka uwaziri wake nyie "wapuuzi"
Like father like son!
 
Makamba kapita picha na Dkt Kalemani ili kusafisha nyota ila bado sana. Mpaka siku atubu kushiriki
Ile haisafishiki hata kwa wale wenzie walioenda kuhiji.
Badala ya alhaji wataitwa aluwaji
 
Back
Top Bottom