Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA) Mkoa wa Mbeya, David Mwambigija, ametoa wito mzito kwa askari wa jeshi la polisi nchini kutojihusisha na matukio ya utekaji wa raia, akisisitiza kuwa wanapaswa kulinda haki badala ya kutekeleza maagizo haramu.
Namnukuu
''Na kufungwa kwa Lissu ndo kujenga nyumba kwa baadhi ya maaskari, mnapoenda kulinda pale mnapata pa dei, sio? Na mikutano hii ya Chadema inavyokuja ndo mnatoka auti na mnabadilisha mboga, sindio? Zamani si walikuwa wanavaa kombati kama zetu maaskari? Siku hizi wamebadilishwa wanavaa hizi hizi za magafikiri kama CCM, sio? Kwa hiyo wana vinasaba na CCM, sio? ''
Anaendelea, lakini ndugu zangu maaskari sikiliza ndugu zangu nyie watoto wa kulima wadogo zetu. Hebu mnapoambiwa maelezo ya juu kwani lazima ufinikishe dili? Ukimpigia simu kwamba nakuja sogea mbele kidogo nitasema hayupo usiku mnaotuteka kwani ukisema dili limefeli shida iko wapi? Kazi kujipendekeza tu.