Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Yanga ili kurithi nafasi ya kocha msaidizi iliyoachwa na Bonfasi Mkwasa alienda kuwa kocha wa taifa stars, tayari mkwasa ameshaaga klabuni yanga. Kocha mkuu wa yanga ndio alie mpendekeza mwambusi kwakua ni mchapa kazi, anajua kukaa na wachezaji na hana majungu.
Kitu Minziro bwana huyo anatetea mashoga akina Nyosso..
Minziro arudi nyumbani aisee!
Kocha Msaidizi wa Yanga atakuwa kati ya Sunday Kayuni au Juma Mwambusi. Mark my words Mkuu. Minziro hatakiwi kwani hana tofauti na Julio hawa Wawili ni Watu wa KUTENGENEZA FITNA na MAJUNGU kwa Kocha Mkuu yoyote wanaekuwa nae katika timu na isitoshe ni MAARUFU MNO kwa kutengeza MATABAKA baina ya Wachezaji. Ukiwa Mtu wa Mpira utakubaliana na hiki nilichokiandika hapa. Na kama wote hao hawatapita basi kati ya Salvatory Edward au Shadrack Nsajigwa mmoja atakamata mikoba ya Mkwasa Yanga kwani hawa ndiyo second selection ya Kamati ya UFUNDI na UONGOZI ya Wasiojua Mpira na watani zangu Dar es Salaam Yanga Football Club a.k.a Wazee wa KUNUNUA.
Kuna kipindi wa mchangani walimtaka Mwambusi. Wakaambiwa huyo ni Yanga damu.
Mwambusi kuwa Assistant Coach Yanga Ni kielelezo cha level ya Yanga kwa sasa. Afanye vizuri mholanzi akiondoka achukue mikoba.
Imedhihirika kuwa ni heri ya kuwa kocha msaidizi wa Yanga a.k.a timu ya kimataifa badala ya kuwa kocha mkuu wa timu kama Mbeya City. Karibu sana Mwambusi Jangwani, tafadhali mwachie maujanja msaidizi wako anipigie Mikia FC katika mchezo ujao.
Wahenga walisema, usiache ubaharia kwa ajili ya unahodha, Mwambusi umeona mbali, pambana hadi utwae mikoba ya Yanga.
kumbe ni mwenzetu..........Kuna kipindi wa mchangani walimtaka Mwambusi. Wakaambiwa huyo ni Yanga damu.
Mwambusi kuwa Assistant Coach Yanga Ni kielelezo cha level ya Yanga kwa sasa. Afanye vizuri mholanzi akiondoka achukue mikoba.