Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MWAMKO MPYA KUHUSU HISTORIA YA BI. TITI
Mwaka jana 2021 kuanzia mwezi October hadi kufika mwezi kama huu na siku kama hizi nilipokea wageni wengi nyumbani kwangu kutoka vyombo vya habari pamoja na CCM wakitafuta historia ya Bi. Titi.
Hakika haya ndiyo maajabu ya Allah kuwa atakapo jambo lake huwa.
Bi. Titi alinyang'anywa mtaa aliopewa kwa heshima yake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na akafutwa katika historia ya TANU kama walivyofutwa wazalendo wengine wengi.
Lakini kwa njia ambazo naamini hata yeye mwenyewe zilimstaajabisha Bi. Titi akarudi katika mwanga akawa anasikika na kuonekana.
Mwaka huu yale ya mwaka jana yanajirudia katika kutafuta historia ya Bi. Titi Mohamed.
Vyombo vya habari vinataka mwaka huu pia kumwadhimisha Bi. Titi Mohamed na kazi kubwa inakuwa kwangu nimweleze Bi. Titi katika namna ambayo itavutia isiwe mambo kuwa yayo kwa yayo.
Ikiwa hivi historia ya Bi. Titi itachusha na kuchosha.
Nawaeleza watafiti wa historia ya Bi. Titi kuwa tusifanye makosa ya wanahistoria waliopita walioandika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kumtaja Nyerere peke yake kama vile TANU haikuwa na wapigania uhuru wengine ila Mwalimu peke yake.
Ukiangalia picha ya kwanza utaona ni Bi. Titi Mohamed na Julius Nyerere wakicheza dansi kusheherekea uhuru wa Tanganyika mwaka wa 1961.
Picha ya pili ni Bi. Halima bint Khamisi na Nyerere miaka mingi baada ya uhuru wakati Mwalimu sasa anaacha uongozi kama Rais.
Wengi watashangaa kusikia kuwa uongozi wa wanawake katika kupigania uhuru wa Tanganyika ulikuwa uchukuliwe na yeyote katika hawa akina mama wawili.
Uongozi uende kwa Bi. Halima au kwa Bi. Titi.
Lakini akina mama hawa kwa ujumla wao ukitaka kujua nguvu yao lazima nikufikishe Viwanja Vya Mnazi Mmoja kwenye mkutano wa TANU mwaka wa 1955 uone walipokuwa wanakaa na nikuhadithie yale waliyokuwa wakifanya katika vibweka kunogesha mkutano.
Angalia picha ya tatu mkono wa kushoto utaona sehemu kuna rangi nyeusi tupu.
Hayo ni mabaibui ya waliovaa wanawake na wamekaa sehemu maalum waliyotengewa wasichanganyike na wanaume.
Picha ya nne nimeiweka makhsusi ili haya mabaibui yaonekane na kufahamika yalikuwaje kwani hivi sasa hayapo kamwe.
Picha hiyo inamuonyesha kulia Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed, na mwanzo kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee na Julius Nyerere ni huyo katikati wanamsindikiza safari ya kwanza UNO Februari 1955.
Jana nilifanya kipindi na TBC nikahojiwa na Dioniz Kidai na hayo niliyoeleza hapo juu ndimo tulimopita katika kueleza historia ya Bi. Titi Mohamed na wazalendo wengine wanawake kutoka majimboni walipogania uhuru mfano wa Bi. Halima Selengia, Amina Kinabo, Mama bint Maalim, Lucy Lameck kutoka Moshi, Shariffa bint Mzee kutoka Lindi, Bi. Zarula bint Abdulrahman na Nyange Bint Chande kutoka Tabora, Bi. Fatuma Matola kutoka Mbeya na wengine wengi