Mwamuzi Omar Artan aliyenyimwa kuingia Marekani kuchezesha Kombe la Dunia apokelewa kishujaa Somalia

Mwamuzi Omar Artan aliyenyimwa kuingia Marekani kuchezesha Kombe la Dunia apokelewa kishujaa Somalia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, amerejea Mogadishu na kulakiwa kama shujaa baada ya kunyimwa idhini ya kuingia nchini Marekani, pigo ambalo litamzuia kuweka historia katika Kombe la Dunia la FIFA la 2026.

Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 34 alikuwa ameteuliwa miongoni mwa waamuzi wa FIFA watakaochezesha mashindano hayo, na alikuwa njiani kuwa mwamuzi wa kwanza kutoka Somalia kuchezesha uwanjani katika michuano hiyo mikubwa zaidi ya kandanda duniani.

Soma: Mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, azuiwa kuingia Marekani, kuchezesha Kombe la Dunia 2026

Hata hivyo, ndoto yake ilizimwa ghafla pale mamlaka za uhamiaji za Marekani zilipomkatalia kuingia nchini humo mara baada ya kuwasili Miami, licha ya kuwa na pasipoti ya kidiplomasia na viza halali ya Marekani ya kuingia mara moja.

 
Ilikuwa ni kuendelea kumpa umaarufu zaidi na kumuongezea fursa
 
Kombe la Dunia la mwaka huu limegubikwa na siasa....
Nina hamu ifike hatua tuone mechi baina ya USA vs Iran au Iran vs Israel
 
Kombe la Dunia la mwaka huu limegubikwa na siasa....
Nina hamu ifike hatua tuone mechi baina ya USA vs Iran au Iran vs Israel
Hakuna raia wa Iran mwenye akili timamu akafurahia maisha nchini kwake Iran. Wote hao ukiwapa nafasi ya kuishi nje ya Iran na ajira hawafikirii mara mbili kukubali hiyo offer.
 
Back
Top Bottom