Kwenye hiyo barua naomba unizungushie duara sehemu ambao imeanisha kosa la mwamuzi ni lipi. Maana imeandika in general kuwa mwamuzi ameshindwa kutafsiri sheria lakini hawakusema sheria namba ngapi iliyoshindwa kutafsiriwa. Na ukiangalia ile mechi ilikuwa na matukio matatu ambalo ni moja kwa yanga na mawili kwa Geita. Kwa Yanga ni kupewa penati. Kwa Geita ni goli lililofungwa mchezaji alikuwa kwenye offside position. Na pia kabla ya kupatikana kwa goli kuna mchezaji wa Yanga alichezewa faulo na kupokwa mpira. Sasa mtu mzima kama wewe unaheshimika na watu humu hupaswi kuongozwa na hisia. Hakuna sehemu ilipoanishwa sheria ipi iliyoshindwa kutafsiriwa