Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia Marekani kwa ajili ya Kombe la Dunia, Omar Artan alikuwa mwamuzi wa kwanza kutoka Afrika kuchezesha fainali ya UEFA Super Cup Agosti 12, 2026 mjini Salzburg, nchini Austria katika Uwanja wa Red Bull Arena (pia unajulikana kama Stadion Salzburg), ambapo klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa.
Juni 6, 2026, ni tarehe ambayo itabaki kwenye kumbukumbu ya Omar Artan milele. Katika siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 34, mwamuzi huyo alipanda ndege kuelekea Marekani akiwa na matarajio ya kuwa Msomali wa kwanza kuchezesha mechi katika Kombe la Dunia la FIFA.
Badala ya kutimiza ndoto yake ya kuiwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia lililofanyika Amerika Kaskazini, Artan alihojiwa kwa takribani saa 11 na maafisa wa U.S. Customs and Border Protection katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami.
Mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, alikataliwa kuingia nchini humo kwa ajili ya Kombe la Dunia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami Juni 6. Hata hivyo Rais wa FIFA, Gianni Infantino, hakuweza kubadilisha uamuzi uliotolewa na utawala wa Donald Trump.
Licha ya kuwa na pasipoti ya kidiplomasia pamoja na visa halali, Artan alizuiwa kuingia nchini humo na kurejeshwa nyumbani ambako alipokelewa na maelfu ya mashabiki na kupokea mwaliko wa kuchezesha Fainali ya CECAFA Kagame Cup, Agosti 7, 2026, ambapo wenyeji Rayon Sports ya Rwanda waliibuka mabingwa kwa kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-1 baada ya kuongezwa dakika 120.
Artan aliteuliwa na UEFA kuchezesha mechi ya Super Cup kati ya Paris Saint-Germain na Aston Villa, na hivyo kuwa mwamuzi wa kwanza wa Kiafrika kuchezesha fainali ya Super Cup ya Ulaya.
kupitia UEFA.com MWAMUZI WA MECHI YA UEFA Omar Artan amesema;
"Ilikuwa kipindi kigumu sana. Watu wengi walinionea huruma kwa sababu mtu anapofanya kazi kwa miaka mingi na kutegemewa kufanya jambo fulani, kisha akashindwa kulifanya, ni changamoto kubwa. Hata hivyo, nathamini sana uungwaji mkono niliopata kutoka kote duniani; nashukuru sana."
Pia, Soma:
Juni 6, 2026, ni tarehe ambayo itabaki kwenye kumbukumbu ya Omar Artan milele. Katika siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 34, mwamuzi huyo alipanda ndege kuelekea Marekani akiwa na matarajio ya kuwa Msomali wa kwanza kuchezesha mechi katika Kombe la Dunia la FIFA.
Mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, alikataliwa kuingia nchini humo kwa ajili ya Kombe la Dunia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami Juni 6. Hata hivyo Rais wa FIFA, Gianni Infantino, hakuweza kubadilisha uamuzi uliotolewa na utawala wa Donald Trump.
"Ilikuwa kipindi kigumu sana. Watu wengi walinionea huruma kwa sababu mtu anapofanya kazi kwa miaka mingi na kutegemewa kufanya jambo fulani, kisha akashindwa kulifanya, ni changamoto kubwa. Hata hivyo, nathamini sana uungwaji mkono niliopata kutoka kote duniani; nashukuru sana."
- Mwamuzi Omar Artan aliyenyimwa kuingia Marekani kuchezesha Kombe la Dunia apokelewa kishujaa Somalia
- Refa Omar Artan aliyezuiwa kuingia Marekani ateuliwa na UEFA kuchezesha Fainali ya Super Cup kati ya PSG na Aston Villa
- Mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, azuiwa kuingia Marekani, kuchezesha Kombe la Dunia 2026
- Refa Omar Artan aliyezuiwa kuingia Marekani ateuliwa na UEFA kuchezesha Fainali ya Super Cup kati ya PSG na Aston Villa