Mwana CCM unazungumzia kupoteza watu wakati sera za chama zimebadilika. Huyu aelemishwa 4R

Mwana CCM unazungumzia kupoteza watu wakati sera za chama zimebadilika. Huyu aelemishwa 4R

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
829
Reaction score
1,120
Nimesikiliza kauli za kijana wa UVCCM huko Kagera akizungumzia kupoteza watu kutokana na kumtukana Rais,na pia nimemsikiliza Dr Nchimbi akipinga kauli hiyo kwa nguvu,kwenye ziara zake.

Kwa mawazo yangu inaonekana bado kuna watu wana mawazo na mitizamo ya mifumo na sera ya awamu ya 5.

Naomba wanachama na watendaji wa chini wa chama na Serikali wabadilike kuendandana na falsafa ya Rais wetu awamu ya 6 waache mambo ya "copy and paste" hii ni awamu nyingine hakuna kupotezana tena utawala wa sheria unatamalaki.

Na ndiyo maana Rais anaendelea kupewa digrii za heshima na mataifa mengi.

Ndugu wasikilize viongozi wako usije ukatolewa kwenye chama kwa kupingana na Mwenyekiti wako. wake up!
 
Usisahau...ndege wafananao huruka pamoja!
 
Back
Top Bottom