Mwana Daresalaam, Fanya hivi unapokabwa na panyarodi.

Hii ni kama nadharia ya kilimo cha matikiti. Ikija vitendo ni hasara tupu.

Likija swala la kuvamiwa haijalishi iwe panya road au paka njia, tafuta nafasi moja ya kujinasua tu. Ikibidi kukimbia kimbia kwa spidi zote, ikibidi kuwapa pesa ama simu wape tu, mwisho wa siku uhai una thamani kubwa kuliko mali.

Ogopa sana watu wa ovyo wakiwa wengi, hao panya road hawaji mmoja mmoja hata siku moja. Sasa hizi kung fu za picha zitaishia kukupatia ngeu tu kama sio umauti.

Kama ilivyo wewe unaevamiwa kuwa na taharuki halkadhalika na hao wavamizi wanakuwa na uoga huo huo, ila wao wanakuwa wameongeza na vilezi kupata ujasiri wa kijinga. Watu kama hao kukupiga sime la shingo ni sekunde tu.

Taekwondo muachie Jackie Chan. Hakuna maiti jasiri, usijidanganye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…