‘Kabla sijatangaza kuna baadhi ya wanaharakati Twitter walishatangaza kwamba nina Corona, wakati nilipotangaza, wakabadili upepo kwamba nafanya kiki, then watu hao hao wakabadilika kwamba napumulia mipira Mloganzila.’ - MwanaFA on XxL
‘Mimi nilikuwa nimewekwa ‘Isolation Centre ya Temeke’, sikuwa Mloganzila, Temeke tulikuwa takribani watu 16, tulikuwa pale wengi tumepona, nadhani wamebaki wawili mpaka sasa.’ - mwanafa live on XXL
‘Wengi wanauliza kwanini nimechukua muda mrefu kupona, changamoto ilikuwa ni kutokana na historia yangu ya kuwa na #Asthma - lakini Alhamdulillah now nimepona kabisa.’ - mwanafa on XXL
‘Kiukweli mimi Corona haikunikuta vibaya, labda huenda kwasababu kinga ya mwili ipo vizuri, na ndio maana nilisema ‘Malaria ni tishio kuliko Corona’, lakini kila mtu ana kinga yake so ilivyonikuta tofauti na watu wengine.’ - MwanaFA #XXL
‘Mimi nimekaa ‘Isolation Centre’ kwa siku 28, nimepimwa mara 8 na mara 7 zote majibu yalikuwa yanarudi Positive, lakini namshukuru Mungu mara 8 wakajiridhisha nimepona 100%.’ - mwanafa on XXL.
‘Kuhusu hisia kwamba niliongopa, siwezi kuwalazimisha kuamini vinginevyo. We unadhani kati ya QChief na Rais MagufuliJP nani ana taarifa zaidi kuhusu Corona? Rais alinipigia na kunipa pole na kunitia imani katika lile janga.’ - MwanaFA on XXL