Mwana FA hajui mnyororo wa thamani katika sherehe za harusi, aelimishwe...

Bangi inaweza kuwa regulated na ikaingizwa kwenye mfumo rasmi kama vileo vingine. Ni moja ya zao zuri la uchumi.

Ni suala la muda tu. Itaruhusiwa.
Kwann liwe swala la muda wakati watu hawana ajira?
 
Kuoa si jambo la dharura kwa wahusika, hata aina ya kuoa, ndoa, na sherehe ni maamuzi yako. Kuchangisha michango ni unyonyaji, utumwa, kuwa omba omba, kujivika kilema, kusujudu, shortcut ya kuwa na nyumba, kiwanja, gari na etc.

Kuchangisha harusi na masherehe ni unyonyaji, tuanze kuchanga kuuguza, kusomesha, kujenga nyumba, hospitali, madaraja, macaravati, mitaro, kuvuta maji, nguzo za umeme, posho za waalimu, madarasa, vyoo.
 
Kuna watu tumesha wachangia ila leo wanasema ni suala binafsi kwA kuwa tu wamesha toka kwenye hili jambo

Wazee hili si suala binafsi ni suala la kijamii kama ilivyo misiba na magonjwa tuendelee kusaidiana (kudumisha undugu) kuwa pamoja na kuleta ukaribu

Kwamba uache kunichangia (makusudi) kwenye sherehe alafu ukipata shida utegemee nijitoe kukusaidia (100%) unaumwa wewe?
Tusaidiane kwenye shida (misiba, magonjwa) na raha (sherehe) sema hii michango ya laki si pesa hapana

Michango ya birthday pia hapana, michango ya mke wa 2 hapana pia
 
Michango ya harusi imefanya gharama ya kufanya sherehe iwe juu sana with the assumption kuwa kila mtu anachangiwa.

Yaani vendors wameweka bei zisizo na uhalisia kiasi kwamba kama unataka fanya sherehe yako bila kuchangisha watu inakucost sana.

I hope itafika wakati tutaacha kuchangiana. Michango ibaki ndani ya familia ya karibu.
 
Ndio ukitaka mbwembwe jipande na ndoa zenyewe zisivyo dumu sasa kama ndoa ya juzi ya manara[emoji849][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Umechanganya mambo. Hayo mambo ya mitaro, madaraja, umeme na mengine ni majukumu ya serikali kutokana na kodi zinazokusanywa.

Suala hili la kijamii na kiuchumi (socio-economy) tunaliweza. Ni letu.
 
michango imezidi sana aisee yaani tungekua kama wenzetu kenya wanaochangia harambee kwaajili ya kusomeshana , ujenzi nk tungekua mbali sana , kibaya zaidi hata hao wanaochangisha wanadai as if ni kitu cha lazima kabisa
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Suala la bei kupandishwa ni law of demand & supply, haiwezi kuzuilika.

Tunaweza kukubaliana namna ya kuchangiana na viwango elekezi, lakini kuona kwamba lote ni jambo lisilofaa hapana kwa kweli.

Hii 'culture' tayari imeshakuwa ni moja ya sekta ndogo ya kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…