Mwana FA hajui mnyororo wa thamani katika sherehe za harusi, aelimishwe...

Kuna raha yake kujumuika na watu wengi unaowafahamu kwenye siku yako muhimu maishani.

Pia msisitizo zaidi upo kwenye mnyororo wa thamani.
Kwani kwa bajeti yako huwezi kuwalipa hao wa kwenye mnyororo? Yaani kutokana na kiasi ulicho nacho

Halafu hapo kwenye kujumuika pamoja siku mkija kugombana na mke/me nguvu yakuwaambia hao watu waliojumuika na wewe kwenye harusi yako kua haiwahusu na wafuate maisha yao utaitoa wapi? Na wakati wao ndo walikamilisha tukio zima la harusi
 
Fikiria kama kila Familia ingejitoa kuchangia ujenzi wa miundombinu ya taifa, leo hii tungekuwa wapi ?

Matokeo yake tumebaki kulia lia na serikali tu
 
Mwana FA hakuchukua mchango wa mtu wakati anaoa. Usi force mambo
 
Watu kushiriki tukio la harusi haiwapi mamlaka katika ndoa yako. Unawazaje?

Ni kweli kama mtu ana uwezo wa kulipia vyote hivyo bila kuchukua hata senti ya mtu ni jambo zuri, lakini sio wote wenye uwezo, ndipo hata wazo l a kuchangishana lilipoibuka.
 
Kwa nini usichangie mwanafunzi anayedaiwa ada ya elfu 50 au laki moja? Kwa nini usichangie omba omba au mgonjwa ambao wana uhitaji zaidi?
Hapo watanionaje kama nimechanga na mimi nataka kuonekana nimechanga
 
Umechanganya mambo. Hayo mambo ya mitaro, madaraja, umeme na mengine ni majukumu ya serikali kutokana na kodi zinazokusanywa.

Suala hili la kijamii na kiuchumi (socio-economy) tunaliweza. Ni letu.
Wewe unalipa kodi ?
 
Yaani mzazi wako akusomeshe halafu ufanye mambo ya kipuuzi shuleni , useme mambo ya shule hayamuhusu, hizo akili au matope
 
mtu asie na uwezo ana uwezo wa kutoa mahari? Au inakatwa kwenye michango?
 
Mwana FA hakuchukua mchango wa mtu wakati anaoa. Usi force mambo
Si anajiweza mkuu, sisi kina pangu pakavu atuache tuendelee saidiana mkuu asilete mawazo yake ya kibwanyenye kwetu (kumbuka Ana mgao wa bilioni kadhaa toka tigo)

Wewe na mimi wa dagaa za mia mia tukisema tufate mawazo ya bwanyenye mwana fa nakwambia tunaenda vunja undugu, urafiki na watu

Kutochangisha yeye haifanyi kitendo hiki kuwa haramu tuendelee changishana harusi ni sehemu ya kujamiiana pia sawa na misiba na magonjwa
 

Mwana fa harusi yake hakuchangisha mtu. Ilikuwa harusi ndogo sana ambayo kila kitu kilifanyika nyumbani.. hakuna cha mc wala ukumbin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…