Mwana FA hajui mnyororo wa thamani katika sherehe za harusi, aelimishwe...


Mkuu natarajia kufunga ndoa mapema hivi karibuni! Tafadhali mchango wako ni wa muhimu sana ili kufanikisha jambo hili!
Tupendane mkuu...
 
Wazaramo wanasema usipohusika kwenye ngoma yamwanangu nakwenye msiba wamzazi wako usinitumaini
 
Naunga mkono hoja ya Mwana FA. Hata mimi sichangii sherehe yoyote.
Nitoe pesa ya mchango,
Nitoe pesa ya nguo sijui sare,
Nitoe pesa ya zawadi,
Bado sijafanya make up,
Hehehehe

Tena usiombee waoane wakiwa washatiana mimba, hujakaa sawa kidogo mtoto kazaliwa upeleke zawadi bado arobaini ya mtoto ukinusurika kuchangishwa basi zawadi lazima, looooh!
 
Upuuzi mtupu.
 
aiseee haya mambo mi huwaga sishiriki kabisa nachangia tu kufanikisha ila msiba hta mkoani naenda kwa gharama yeyote
kwa nn naona ni mambo ya showoff tu kelele gharama kibao za harusi final haina tija mi nilikataa since graduation ya form 4&6 mpaka chuo napenda mtu afanyiwe hata kumchangia kama uwezo ninao ila mm siwezi kabisa
hata siku nikioa nataka ile kimya kimya sherehe mi labda nshaondoka
 
Suala sio kujiweza, suala mnapenda show off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…