Mwana FA hajui mnyororo wa thamani katika sherehe za harusi, aelimishwe...

Huu ulazima unatoka wapi?

Hii tabia ya kuchanga ili uchangiwe inaharibu wengi.
 
Marafiki/Ndg/Watu wa karibu yetu wanataka kuoa wanatamani kufanya sherehe nzuri ilhali hawana uwezo wa kufanikisha wanachokitaka wanaomba tuwasaidie kuwachangia waongezee walipokwama hilo ni tatizo?? binafsi sioni tatizo kwenye hilo
 
Mwezi wa 10 nilikuwa Nina kadi 2

Nimechanga moja ingine nimechinjia baharini

Nimeangalia mahusiano yangu na hao wahusika

Infact sipendi michango kabisa .

Unaweza shangaa kiutani utani mwezi mzima unatoa 250k hivi hivi

Kama itakuja tokea nikaoa nitajikusanya mwenyewe nimalize kila kitu bila kusumbua mifuko ya watu
 
Mimi sijawahi kupinga michango kwa shughuli yoyote ya kijamii.

Na kama inavyotajwa ni kweli ni jambo binafsi, lakini tuangalie zaidi Jamii kukutana na kufurahia pamoja...na si kusubiri kukutana wakati wa matatizo tu.

Muhimu ni kuwakumbusha Watu kukumbuka pia kuchangia shughuli kama matibabu n.k.

Pia shughuli hizi hutengeneza ajira kwa kada tofauti sambamba na kusisimua uchumi kwa wanaokodisha kumbi, wanaotengeneza na wanaouza Vinywaji, Nyama, Mchele n.k.

Sioni tatizo labda jamii tu wakumbushwe kuangalia mifuko ya wale wanaodaiwa michango ili wasiumie kwa kuwekewa viwango wasivyovimudu.
 
Umeiweka vizuri sana.

Halafu ukichunguza wanaopinga michango kwa mbwembwe humu, usikute ndio mahodari wa kuchangia mpaka vigodoro.

Tukubaliane kwenye utaratibu na viwango vya michango. Iwe ni hiari pia na sio deni.

Aidha michango iendelee ili tuzidi kusisimua uchumi wa mtu mmoja mmoja waliomo katika mnyonyoro wa thamani wa hizi sherehe.

Tufunge mjadala?
 
Kwani ukijigharamia hizo gharama za harusi hao uliowataja hawapati ajira sijui ma mc, wapishi nk?
 
Mkuu mie harusi yangu Jumla tulikua watu 6, yaani mimi, wife, mashahidi 2(Mke na Mume), DAS na Msaidi wa DAS. Na sitakagi usumbufu kabisa linapokuja swala la michango iwe ndugu or jamaa wa karibu. Najituma na kutoa zaidi katika wagonjwa na Misiba, kwenye misiba hapo hadi nasafiri kabisa pia.

Hoja yangu ni kwamba, harusi sio bahati mbaya watu wajiandae wamalize mambo yao wenyewe. Uki'complicate ndio inakua gharama. Mimi harusi yangu jumla ili gharimu TZS 50,000 ya kuandikisha tuu, Mavazi, sijui viatu nilitumia ambavyo nilikua navaa siku zote same to wife.
 
Sherehe sio lazima mkuu. Anaweza funga ndoa vizuri kabisa bila ya sherehe kama uwezo ni mdogo.
 
Mi naona ni bora kuchangia harusi kuliko msiba, mtu akifa akazikwe tu na maisha yaendelee, harusi tuchangie tufurahie maisha
 
Huyu jamaa nimshamba sana ndio maana wenzake wanasema anaringa,kupata kidegree kimoja anajiona ni professor ni bogus tu na misemo yake ya yakujifanya highly conscious..

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kibingwa zaidi mkuu
 
Hata Mimi namuunga mkono ...sikuchangisha MTU harusi yangu.... Mkioana tuwachangie mnapoachana mnatuitaga kuchanga tushangilie kuachana kwenu !!?? Nilioa na sherehe nikafanya kwa kiwango cha kipato changu inatosha ..... Sikuacha madeni, magomvi kugombana na watu eti uliwachangia nao wakuchagie.... Ujinga sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…