Mwana FA hajui mnyororo wa thamani katika sherehe za harusi, aelimishwe...

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Najua Hamisi Mwinyijuma au Mwana FA ni miongoni mwa wasanii wachache wasomi tulionao hapa Tanzania.

Ukiwa msomi, tunatarajia uwe na fikra pana na za kina kwenye masuala mbalimbali ya kijamii na mazingira yanayokuzunguka, ukiachana na yale ya fani uliyosomea.

NATAKA KUSEMA NINI?

Nimeona video fupi ikisambaa inayomuonesha MwanaFA akizungumzia suala la michango ya harusi. Kwamba, yeye hachangii harusi kwani ni suala la mtu binafsi na linahitaji maandalizi. Yuko tayari kuchangia Msiba, si harusi.

Kwanza, huo ni mtazamo unaofikirisha lakini pia ni mtazamo wa watu wengi. Watu wamechoka na utaratibu wa kuchangia harusi. Mimi ni mmojawapo [emoji2]

Hata hivyo, nikiangalia mnyororo wa thamani uliopo kwenye hizi sherehe na ajira zilizozalishwa, nabaki kuona ni jambo zuri na lenye tija.

Ukichangia harusi, unatoa ajira kwa watu wengi sana. Kuanzia MC, watu wa mapambo, chakula, wapiga picha, maids, watoa burudani n.k.

Faida nyingine ni mzunguko wa fedha kuchochea uchumi wa eneo husika, kuimarisha undugu na ujamaa, kutengeneza kumbukumbu na mengine mengi.

Wapo wasiochangisha watu kwenye mambo ya sherehe, lakini hao ni wale wanaojiweza, vipi wale wasiojiweza?

USHAURI WANGU

Tusiache kuchangiana kama tunapendana na kushirikiana. Umoja ni nguvu. Sherehe za harusi sio suala binafsi tena, ni suala la kiuchumi na maisha ya watu wengi yanategemea hapo.

Mwezi wa 6 mwakani nafunga ndoa. Nitatoa kadi za michango. Mnichangie. Puuzeni maneno laini laini ya Hamisi.
 
MWANA FA IS FUCKN RIGHT, YOU AINT
 
Back
Top Bottom