Mwana FA: Uwanja unaojengwa Arusha utakuwa na uwezo wa kudumu miaka 130

Mwana FA: Uwanja unaojengwa Arusha utakuwa na uwezo wa kudumu miaka 130

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema kuwa uwanja wa mpira wa miguu wa Arusha utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kudumu miaka 130 huku ukiwa unafanyiwa marekebisho kila baada ya miaka 10.

Mwinjuma ameyasema hayo Machi 13, 2025 wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo walipotembelea mradi wa uwanja huo kwa ajili ya kujionea maendeleo yake

Aidha ameongeza kuwa mradi huo umefikia asilimia 33 na utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 32,000 utakapokamilika ifikapo Juni 2026.
 
Akili kisoda hawa Wabunge wa Magufuli hopeless kabisa. Baada ya hiyo miaka 130 itakuwaje?
 
Wajenge viwanja angalau vya kuchukua mashabiki elfu 60.

Waangalie Projection ya Mbeleni.
Waangalie kesho sio Leo tu.

Baada ya miaka 30 kiwanja kitaonekana takataka kama Sokoine, jamuhuei, kirumba nk.

WATUMIE KODI ZETU VIZURI
HIZO NI HELA ZA WATANGANYIKA.
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Anajua uwanja wa Mkapa umefungiwa huyu na haujafika hata miaka 30
 
Back
Top Bottom