Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
-
- #41
Achana naye huyo. Kwa kumsaidia tu ni kuwa hata Rahabu aliyekuwa kahaba alikuja akaleta ufalme katika uzao wake ulioendelea huko. Maana yeye alimzaa Boaz na Boaz akamzaa Obed na Obed akamzaa Yesse na Yesse akaja kumzaa mfalme Daudi.ambaye huyo mfalme Daudi alikuwa mdogo kati ya ndugu zake na alikuwa akichunga kondoo tofauti na kaka zake kama vile Eliabu ambao walikuwa jeshini .lakini Mungu alimuinua Daudi aliyekuwa anachunga kondoo na kumpa ufalme.TAtizo umeamua kumdharau
Yeyote anaweza kua yeyote kwa wakati wowote.
Angalia hata kuinuliwa kwa Samweli mtoto wa Hana aliyekuwa Tasa na ambaye alikuwa anadharauliwa sana na penina ambaye yeye alikuwa anazaa watoto.kwa hiyo usimdharau mtu hata siku moja.imeandikwa ya kuwa.
Mungu humuinua mnyonge kutoka mavumbini ,humpandisha mhitaji kutoka jaani ili kumketisha pamoja na wakuu .
usimdharau mtu kwa namna unavyomuona leo.