TANZIA Mwana JamiiForums Miguu ya Kuku/ Mpauko afariki dunia

TANZIA Mwana JamiiForums Miguu ya Kuku/ Mpauko afariki dunia

Mimi pia nina tatizo kama lake ( kutosikia vizuri) .nilitumia hali hiyo kumpa moyo kila namna kwamba it's OKAY.nilikuwa nampa maneno ya kila namna kumuongezea nguvu ya mapambano ya maisha.but alikuwa na moyo mwepesi mnoo.amenisikitisha sana kwa maamuzi aliyochukua.nimejikuta namwaga chozi kutwa nzima leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Honestly Hakuna chochote cha maana ulichokua ukimpa, acha unafki
 
The guy was so charming
Japo hatukuwahi kuonana lakini alikua mtu wa karibu sana kwangu

Siamini 😭😭😭😭😭😭😢😢😢😢😢😢
 
Mungu wangu!!!!
Huyu member alikuwa kweli ana matatizo ya kusikia.
Na kuna rafiki humu alikuwa anamuunganishia kazi ya ualimu akamsafirisha toka mkoani mpaka alipokuwa rafiki akafanya interview.
Lakini yule rafiki akaniambia jamaa ni shida sana kuongea nae na kufundisha itakuwa ngumu lakini akampa nauli na kumuahidi shule ikifunguliwa basi itabidi aje wampe probation kama ya mwezu kuona kama ataweza lakini kama asipoweza atamsaidia kivingine hapa sikumbuki alisema hearing aids au sijui nini sikumbuki kwa kweli
Kiukweli sijui ni nini nikajikuta namshawishi yule rafiki ampe nafasi kwani hata mimi nilifundishwa na mwalimu kipofu Advance level na ni mwalinu pekee aliyekuwa anasikilizwa na wanafunzi akaeleweka, ni mwalimu bora kabisa.
Rafiki yule alikuwa busy busy nami busy sana basi hatukuongelea ishu ya huyu mpaka sasa.
Mda huu ninaona hapa amejiua.
Aiseeee nimesikitika sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Nahisi sie huyu mkuu. Ni watu wawili tofauti
 
Wale wenzetu wanaokujaga huku kuomba msaada wa ada mfano @najanaja tukiwa nacho tuwasaidie kama hatuna tusiwaseme vibaya (wamekuwa wakitolewa maneno makali wengine wanadiriki kusema wasiombe watafumuliwa marinda).

Hauwezi kujua huo msaada wako anauhitaji kiasi gani na pengine ungemuokoa na maamuzi ya kujiua au hayo maneno yako ya kejeli yangempelekea ajione si kitu aamue kujiua.

Watu wengi wanaojiua ni mapenzi au hali ngumu za maisha. Tujifunze kumsaidia mtu akiwa hai. Sio hadi afe ndio tuanze kusema "hata mimi alinifuata pm ningejua ningemsaidia, au hata Mimi niliona Uzi wake nikajua ni utani.".

Ni kweli wengine wanaomba misaada wakiwa wana nia mbaya na wengine ni kweli ana shida. Ukibarikiwa moyoni saidia na usipobarikiwa kumsaidia epuka kumtolea maneno ya kejeli.

Leo kuna watu wakisikia Najanaja kajinyonga kwa sababu alishindwa kuendelea na masomo na hata biashara alizotamani kufanya alikosa mtaji, watu wataishia kusema " ningejua ningemsaidia". Kama upo kwenye nafasi ya kumsaidia mtu msaidie usisubiri afe ujilaumu.

NB. Kuna watu pia watasema Mimi ni Naja naja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila sema tu kwa sababu ya hiyo depression aliyokuwa nayo lakini kujinyongea nyumbani kwa mtu aliyeamua kumsaidia kama msamaria mwema haijakaa vizuri. Amemwachia mtihani na usumbufu mkubwa ambao unaweza kumfanya ajutie kuishi nae na majuto hayo yanaweza hata kumfanya akafikia uamuzi wa kutokuja kumsaidia tena mhitaji mwingine kwa kiwango kama hicho alichomsaidia huyo aliyejiua. Yaani aliamua kumwachia msala huyo msamaria mwema.
This is very true.
 
Back
Top Bottom