TANZIA Mwana JamiiForums Miguu ya Kuku/ Mpauko afariki dunia

TANZIA Mwana JamiiForums Miguu ya Kuku/ Mpauko afariki dunia

Nimefikiria sana hili na kujaribu kuvaa kiatu cha huyu mama msamaria mwema dah!
Dunia ina mingi mitihani
Mungu amfariji sana huyu mama na familia yake.
Ila sema tu kwa sababu ya hiyo depression aliyokuwa nayo lakini kujinyongea nyumbani kwa mtu aliyeamua kumsaidia kama msamaria mwema haijakaa vizuri. Amemwachia mtihani na usumbufu mkubwa ambao unaweza kumfanya ajutie kuishi nae na majuto hayo yanaweza hata kumfanya akafikia uamuzi wa kutokuja kumsaidia tena mhitaji mwingine kwa kiwango kama hicho alichomsaidia huyo aliyejiua. Yaani aliamua kumwachia msala huyo msamaria mwema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale wenzetu wanaokujaga huku kuomba msaada wa ada mfano @najanaja tukiwa nacho tuwasaidie kama hatuna tusiwaseme vibaya (wamekuwa wakitolewa maneno makali wengine wanadiriki kusema wasiombe watafumuliwa marinda).

Hauwezi kujua huo msaada wako anauhitaji kiasi gani na pengine ungemuokoa na maamuzi ya kujiua au hayo maneno yako ya kejeli yangempelekea ajione si kitu aamue kujiua.

Watu wengi wanaojiua ni mapenzi au hali ngumu za maisha. Tujifunze kumsaidia mtu akiwa hai. Sio hadi afe ndio tuanze kusema "hata mimi alinifuata pm ningejua ningemsaidia, au hata Mimi niliona Uzi wake nikajua ni utani.".

Ni kweli wengine wanaomba misaada wakiwa wana nia mbaya na wengine ni kweli ana shida. Ukibarikiwa moyoni saidia na usipobarikiwa kumsaidia epuka kumtolea maneno ya kejeli.

Leo kuna watu wakisikia Najanaja kajinyonga kwa sababu alishindwa kuendelea na masomo na hata biashara alizotamani kufanya alikosa mtaji, watu wataishia kusema " ningejua ningemsaidia". Kama upo kwenye nafasi ya kumsaidia mtu msaidie usisubiri afe ujilaumu.

NB. Kuna watu pia watasema Mimi ni Naja naja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Changamoto ni namna gani ya kuthibitisha yupi tapeli yupi mwenye shida ya kweli. Kumbuka Kuna watu wametapeliwa humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rest in Peace brother Robin.

Sijaamini kama umejiua rafiki yangu.

Ndugu zangu hasa wenye mizaha, tujifunze kutunza ndimi zetu na kuchunguza maneno yetu, hasa pale tunapoyatoa kwa mtu anayehitaji msaada wetu, kuna binadamu wenzetu wanapitia hali ambayo uchungu, adha na maumivu yake ni magumu sana kuelezeka na kueleweka kwa mtu ambaye hajawahi pitia hali husika.

Upumzike mahali pema peponi kaka yetu.
 
Behave pls...!mimi kwangu sina mtoto mlemavu wa akili...na huyu mama ni mtu mzima usitake tuharibu uzi[emoji57][emoji57]
Huyu mama better asijitokeze tu watu Wa Jf hawatohesabu wema wake Bali wataleta kashfa na mizaha
Najaribu vaa kiatu cha huyo mama hakinitoshi kabisa, unajitoa kumsaidia MTU kisha anajinyongea nyumbani kwako
..
Mungu amfariji na familia yake pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeumia Sana.
Nimekumbuka alishawahi nipm sikujua Kama ni mpauko..kumbe alikuwa akitumia jina la miguu ya kuku.
Nilimjibu baada ya mwezi kupita lakini hakunijibu Tena.
Na Mimi akili ya kufwatilia japo posts zake Sikuwa nayo..laiti ningejua Kama miguu ya kuku ndiye huyo mpauko basi ningefanya bidii zaidi kumtafuta japo kuongea naye.
Mungu nirehemu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mpendwa msiba umetugusa wengi
 
Huyu mama better asijitokeze tu watu Wa Jf hawatohesabu wema wake Bali wataleta kashfa na mizaha
Najaribu vaa kiatu cha huyo mama hakinitoshi kabisa, unajitoa kumsaidia MTU kisha anajinyongea nyumbani kwako
..
Mungu amfariji na familia yake pia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na mm nahis alifanya madhira haya kwa huyu mama...! Maana ni siku chache toka awasiliane na ss...rip...!
 
Mimi pia nina tatizo kama lake ( kutosikia vizuri) .nilitumia hali hiyo kumpa moyo kila namna kwamba it's OKAY.nilikuwa nampa maneno ya kila namna kumuongezea nguvu ya mapambano ya maisha.but alikuwa na moyo mwepesi mnoo.amenisikitisha sana kwa maamuzi aliyochukua.nimejikuta namwaga chozi kutwa nzima leo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na mm ndo nilimdirect kwako..alikua hajui.nikambaia akusearch akaja akanianbia mwenzangu ni tajiri dah ..alishakata tamaa ..nadhan familia yake imechangia dah
 
Huyu mama better asijitokeze tu watu Wa Jf hawatohesabu wema wake Bali wataleta kashfa na mizaha
Najaribu vaa kiatu cha huyo mama hakinitoshi kabisa, unajitoa kumsaidia MTU kisha anajinyongea nyumbani kwako
..
Mungu amfariji na familia yake pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mama mwenye mji alipojinyongea Mpauko ndiye mwenye mtoto mwenye ulemavu wa akili? Na huyo mtoto mwenye ulemavu wa akili amechangia nini kwenye tukio la jamaa kujiua? Sijaelewa ile comment ya Wangari Maathai pale juu kwenye post # 181.
 
Nimeumia Sana.
Nimekumbuka alishawahi nipm sikujua Kama ni mpauko..kumbe alikuwa akitumia jina la miguu ya kuku.
Nilimjibu baada ya mwezi kupita lakini hakunijibu Tena.
Na Mimi akili ya kufwatilia japo posts zake Sikuwa nayo..laiti ningejua Kama miguu ya kuku ndiye huyo mpauko basi ningefanya bidii zaidi kumtafuta japo kuongea naye.
Mungu nirehemu

Sent using Jamii Forums mobile app

Ila tumetofautiana...mm had mtu aje pm najua ni timamu..lazima nireply aise! Tusipende kidharau mambo hata km madogo..tubu! Na badilika
 
Back
Top Bottom