Ungeziona posts zangu za zamani wewe! Dadeki, mtu wakati wa kunisoma akiwa na kichwa kibovu; anaweza kupotea within a paragraph halafu asijue aliyokuwa anasoma ni para ya juu, ya chini yake au ndo hiyo hiyo anayoikodolea macho!
Mi nadhani wengine tumejaaliwa kipawa cha kuandika! Once you click a single key on the keyboard, maneno yana-flow tu on their own... ukija kushituka; umejaza ma-page!
Nina hilo tatizo hadi kesho! Hapa nilipo nina kipolo cha
zitto junior kwenye thread ya Nyani Ngabu!
As usual, baada ya kugusa tu keyboard... vidole vikaanza kutiririka tu; kuja kushituka, Hamad! Napeleka kwenye MS Word ili kujua words count, nakuta nimegonga kwenye 1456 words halafu vidole bado vina genye ya kuendelea kutiririka!
Hapa nilipo nipo kwenye kibarua cha kuifupisha na kuipangilia ili ku-meet "JF Standard!" Standard ya wavivu wa kusoma!
Tena eh! Leo hapa nimetoa siri yangu!
Ukiona nachelewa kujibu post tu; jua kama ni kuandika, nishaandika zamani lakini words count ipo kwenye 6589 halafu naona duh!! Hii sasa too much!!
Afu Mungu bhana, anaacha kutupa vipaji vya akina Diamond Platnumz, ingekuwa tunawatafuna tu hivi sasa akina
Demiss, kiulainii bila kuhitaji msaada wa akina
Mwifwa!! Kinyume chake, tunashushiwa zigo ambalo hata totoz wenyewe linawaboa; aaaaaaargh!!