POTOSHI Mwanaanga Christina Koch apeperusha bendera ya Ghana kwenye misheni ya Artemis 11

POTOSHI Mwanaanga Christina Koch apeperusha bendera ya Ghana kwenye misheni ya Artemis 11

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1775958023053.png
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na Picha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa instgram , facebook na x ikimuonyesha mwanaanga Christina Koch akiwa ameshikilia bendera ya taifa la Ghana wakati wa mission ya artemis II. Picha hiyo imevutia watu wengi zaidi kutokana na historia ambayo imeandikwa na mwana Anga huyo kuwa mwanamke aliyeshiriki kwenye misiion ya Artemis II

Kwa kutumia utafutaji wa maneno mhimu, unaonyesha kuwa picha hiyo ilipigwa mnamo Desemba 2019 wakati Koch alikuwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga (ISS)

Sambamba na hilo Christina Koch mwenyewe alichapisha picha ya bendera kwenye ukurasa wake wa X zamani twiter mnamo Desemba 12, 2019, akielezea uzoefu wake wa kusoma Chuo Kikuu cha Ghana miaka 20 iliyopita na kuonesha upendo wake kwa nchi hiyo. Katika chapisho lake alisema,

"Miaka 20 iliyopita, nilikuwa nasoma nje ya nchi katika Chuo Kikuu cha Ghana (@UnivofGh). Kama ilivyo safari ya kwenda anga za juu, ilikuwa ni uzoefu chanya uliobadilisha maisha yangu na kunipa mtazamo mpana zaidi. Kuona uzuri wa Ghana kutoka angani kunanikumbusha watu wa ajabu niliokutana nao huko, na jinsi tunapochunguza dunia, tunavyojifunza zaidi kuhusu sisi wenyewe."

Kwa kuzingatia hivyo picha hio ni halisi ila haoneshi kuwa tuio la hivi karibuni ambalo limeshuhudia mwana anga huyo akianza safari yake ya artemis II ambayo ilizinduliwa April 1 2026 na kutamatika 10 April

Kwa sasa, hakuna picha rasmi au ushahidi wowote unaothibitisha kuwa Christina Koch aliibeba au kuonesha bendera ya Ghana wakati wa misheni ya Artemis II. Ueneaji wa taarifa hii si sahihi unaonekana kuendeshwa na historia ya mwanaanga huyo na Ghana, pamoja na upendo wake kwa nchi hiyo.
Licha hilo tovuti rasmi ya NASA ilichapisha baadhi ya vitu mhimu ambavyo Nasa imeorodheshwa kuchukuliwa katika safari hiyo na mamabo ambayo yanajumuishwa katika safari hiyo

Aidha Rais wa Ghana, John Dramani Mahama, amempongeza Christina Koch kwa nafasi yake ya kihistoria kama mwanamke pekee kwenye misheni ya Artemis II​

Attachments

  • images (1).jpg
    images (1).jpg
    12 KB · Views: 32
Back
Top Bottom