TANZIA Mwanachama na mfanyakazi wa JamiiForums, Dotto Mnzava afariki dunia kwa ajali ya pikipiki

Status
Not open for further replies.

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285








Jamii Media Limited inasikitika kutangaza kuondokewa na mmoja wa wafanyakazi wake, Mwandishi Mkuu wa FikraPevu.com, Dotto J. Mnzava aliyefariki leo, Disemba 14, 2015 kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki na gari iliyotokea maeneo ya Victoria, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.


Mnzava alikuwa mwandishi wa Habari akiiandikia mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com na alijiunga na Jamii Media mapema mwaka jana, 2014.


Mipango ya mazishi na kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea kwao Same kwa ajili ya maziko inaendelea kufanyika na kwa sasa mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Kuaga mwili kwa wakazi wa Dar kutafanyika Disemba 16, 2015 katika Kanisa la Waadventista Wasabato, Manzese (ulipo uwanja wa Tippi).


Tunatoa pole za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dotto J. Mnzava.

Mungu amjalie pumziko la amani!


Amina

===================

Habari toka vyanzo vingine zaidi:




===================

UPDATE:
Habari za jioni WanaJamiiForums,

Mwili wa ndugu yetu Dotto Mnzava tayari umeagwa rasmi kwa hapa Dar-es-Salaam katika Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese karibia na uwanja wa TIPPI.

Mwili wake uko njiani unasafirishwa kuelekea nyumbani kwao Same Kilimanjaro kwa ajili ya kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Tunaendelea kuwakaribisha rafiki na ndugu wote wa Dotto Mnzava tuungane tukielekea kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele.

Kwa maelezo zaidi piga namba: 0767 137 137
=====================


 

Attachments

  • Dotto_Mnzava_Pavillion.jpg
    31.5 KB · Views: 10,603
  • index.jpeg
    27.5 KB · Views: 4,807
HABARI

Nimepokea taarifa za kushtua na zenye simanzi ambayo ni ngumu kufutika kichwani, tumempoteza kipenzi chetu, mwenzetu na rafiki yetu Dotto Mnzava. Dotto ni mwandishi wa habari na alikua anaenda kwenye mishe zake za kikazi. Kutokana na foleni za Dar ikabidi achukue boda boda. Akiwa eneo la Victora, pikipiki aliokuwa akisafiria ilipata ajali na yeye alianguka barabarani ndipo gari ikampitia kichwani na kusababisha mauti yake.

BWANA AMETOA NAYE AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
 

Attachments

  • profilepic213201_2.gif.png
    85.6 KB · Views: 11,497
Wakuu kuna taarifa zimeenea kuwa member mwenzetu Dotto Mnzava kafariki kwa ajili.

Mwenye taarifa rasmi tunaomba kujulishwa.
 
Last edited by a moderator:
HABARI

NIMEPOKEA TAARIFA ZA KUSHTUA NA ZENYE SIMANZI AMBAYO KUFUTIKA KWAKE KICHWANI HAKUTAISHA KAMWE
TUMEMPOTEZA KIPENZI CHETU MWENZETU RAFIKI YETU Dotto Mnzava INAUMA SANA YANI HATA MPAKA SASA
SIAMINI KWELI DOTTO AMETUTOKA HIVI; NASHINDWA HATA KUANDIKA HAPA
AMEFARIKI MAENEO YA VICTORIA KWA AJALI YA PIKIPIKI, TAARIFA KAMILI TUTAZIPATA KUTOKA KWA NDUGU ZAKE NA WALE WALIOKARI NAYE


MUNGU AWAPE FARAJA NA KUWAPA NGUVU FAMIILIA ALIYOIACHA, NDUGU PAMOJA NA
UONGOZI WOTE WA JAMIIFORUM

BWANA AMETOA NAYE AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE




 
Wapendwa wana Jf, ni masikitiko makubwa kuwajulisha kifo cha member mwenzetu hapa Jf Dotto Mnzava kilichotokea leo mchana saa 8 baada ya kupata ajari ya Pikipiki maeneo ya Victoria jijini Dar.


Mwili wa marehemu umehifadhiwa ktk hospital ya mwananyamala kusubiri taratibu zitakazofata.

Pumzika kwa amani rafiki yangu Dotto.
 
Last edited by a moderator:
Tumechoka na hawa watu wa yellow journalism, mada yakikuda hii.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…