TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

condolences kamanda mtoi,s family, ni pigo kwa wanamabadiliko.

So sad Mungu amlaze mahali pema na ampokee ndugu Mtoi. ..Bwana Ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe..Mungu awape faraja na nguvu wanafamilia katika kipindi hiki kigumu sana wanachopitia
 
Kila nafsi itaonja umati nimepokea kwa maskitiko makubwa taarifa za kifo cha kamanda wetu mohamed Mtoi hakika hapa duniani sekunde moja tuu inatosha kubadilisha jina wapendwa wana JF jiwekeni tayari na kujiandaa muda wowote kurudi kwa baba yetu poleni sana wafiwa wote.Raha ya milele umwangaze Mungu apumzike kwa amani.Amen.
 
Last edited by a moderator:
Pole zangu zifikie ndugu na jamii yote pamoja na chama chetu kipenzi cha chadema na wana mapambano wote,kwakweli inauma sana ila tuseme Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake na libarikiwe
 
Mwenyezi Mungu awape nguvu familia yake na akupumzishe pema peponi Insha'Allah. Angalizo naomba chadema msiutumie msiba huu kujijenga kisiasa mtakuwa hamjatenda haki kwa marehemu.
 
Dah!...it's hard to believe this really,kwa hakika hili ni pigo kubwa sana kwa #UKAWA ...Mwenyezi mungu ampumzishe mahali pema huko aendapo!
 
Rest In Peace Mohammed Mtoi
Umetangulia! Hio ni Safari ya wote
 
Kwenye facebook niliona likes kuhusu kifo cha mtanzania mwenzetu, sikuweza kuelewa walimaanisha nini haswa. RIP
 
RIP Mtoi. Pole kwa familia na kwa Chadema pia. Mungu akupeni ujasiri na ustahimilivu ktk kipindi hiki kigumu.
 

Ni Lazima uchunguzi ufanyike. wataalamu wa ajali waliangalie hilo gari kwani inawezekana hii ni foul play. Binafsi sio mtaalamu wa ajali lakini nikiangalia hiyo gari ninashindwa kuelewa inakuwaje vioo vya dirisha viharibike kiasi hicho bila frame zake kuwa na hata chembe ya kupindika! I am just wondering!
 
Inauma sana Mkuu...wacha kamanda apumzike kwa amani sema kamanda unajua nini?? Tuwe na mashaka na MA-CCM kwa kifo cha kamanda wetu si unajua sisi hatuamini katika Mungu...kila kitu sisi tunakomaa tu kwamba ni Ma-CCM #RIP brother Mtoi
Hicho kilevi unachotumia acha mara moja.unakoelekea ni kurukwa na akili bwanamdogo.
 
Pumzika kwa Amani Mtoi.

Mchango wako kwenye Taifa hili utakumbukwa daima.
 
R.I.p kamanda hutasahaulika ndani ya mioyo yetu. Mungu akulaze pema peponi .
 
Imenisikitisha sana,ametutoka Mtoi!Mungu mrehemu marehemu
 
Nimeshtushwa sanaa na hii habari.....
Kamanda mtoi nimeshirikiana sana na wewe katika harakati zoteeee, why this happened at this time??

Mungu namwombea Kamanda Mtoi apate punziko la amani.

Mungu wape faraja familia, ndugu na jamaa wa Mtoi, Mbele yetu ,nyuma yako.

R.I.P MOHAMMED MTOI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…