Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeumizwa sana na kifo hiki!.
Ama kweli nimeamini yanayosemwa na watu, "wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana!".
Ila Tanga nako....!, na hizi ajali za kuelekea chaguzi!....
Nimeikumbuka ajali ya Marehemu Juma Jamaldin Akukweti, ambayo ilitokea kuelekea uchaguzi!, ilikuja kusemekana kuna mkono wa mtu katika kugombea jimbo!, na huyo mtumiwa, japo alilitwaa hilo jimbo, lakini hakuchukua round, tena yeye aliondoka kwa mateso makubwa!.
Kama ni ajali ya kawaida, Mungu amrehemu marehemu!, lakini kama ni mkono wa mtu, subirieni 'karma' reaction soon, karma haikopeshi wala haiongopi!.
Poleni sana wafiwa, poleni Chadema!, poleni wana jf, tumempoteza sio tuu mwana jf mwenzetu, bali mpashanaji habari mahiri!.
RIP Kamanda Mtoi!.
Pasco
Mwehu baba yako aliyekufundisha adabu mbovu. Hapa topic ni msiba bangi na viroba mbele ya safari
R.I.P Pigo kwa Chadema na makamanda wapenda mabadiliko wote. Mtoi hakuwahi,hajawahi na hakuwa msaliti. Na alipambana mpaka tone la mwisho la damu yake. Mods kama itawapendeza na kama utaonekana umuhimu uanzishwe uzi maalum kwa ajili ya ku pay tribute kwa Kamanda Mtoi. Tujikumbus hebposts zake muhimu. Pia utaratibu wa kufikisha rambirambi kwa familia yake kama mwana JF.
Nimelia sana sana, tuliongea juzi. Kwanini afe yeye tu? Hapana aiseee. Nimelia sana tulikua pamoja, Mama yake ndio Mama yangu, familia yake ndio yangu, tukipokuwa shambalai tuliamua kuhamia wote kwenda Magamba school. Why?