Nimeumizwa sana na kifo hiki!.
Ama kweli nimeamini yanayosemwa na watu, "wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana!".
Ila Tanga nako....!, na hizi ajali za kuelekea chaguzi!....
Nimeikumbuka ajali ya Marehemu Juma Jamaldin Akukweti, ambayo ilitokea kuelekea uchaguzi!, ilikuja kusemekana kuna mkono wa mtu katika kugombea jimbo!, na huyo mtumiwa, japo alilitwaa hilo jimbo, lakini hakuchukua round, tena yeye aliondoka kwa mateso makubwa!.
Kama ni ajali ya kawaida, Mungu amrehemu marehemu!, lakini kama ni mkono wa mtu, subirieni 'karma' reaction soon, karma haikopeshi wala haiongopi!.
Poleni sana wafiwa, poleni Chadema!, poleni wana jf, tumempoteza sio tuu mwana jf mwenzetu, bali mpashanaji habari mahiri!.
RIP Kamanda Mtoi!.
Pasco