TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

Daah!!!
Mungu amlaze mahali pema.
Ninaamini kifo chake ni kwa mapenzi ya Mungu na nawapa pole sana wafiwa.

Mapambano na yaendelee
 
..habari hizi zimenishtua.

..mara kwa mara nilikuwa nawasiliana na Mohamed hapa jf kwenye private message.

..bahati mbaya ujumbe wangu wa mwisho alikuwa hajaujibu, kwa hiyo wiki hizi mbili nilikuwa najiuliza sana kuhusu huyu ndugu yetu.


..then zinakuja habari kwamba ametutoka!! yaani hata sijui niseme nini.

..REST IN PEACE MOHAMEDI MTOI.
 
RIP mohamed Mtoi..
Nilikutana na huyu jamaa tar 15/2/2015 pale Corridor springs hotel, Arusha kwenye mkutano wa wadau wa CDM kanda ya kaskazin. Asee jamaa alitugusa sana kwa namna yake ya kuongea na kujenga hoja. Mungu akurehemu bro.
 
Last edited by a moderator:
Inabidi nikubali tu kuwa huo ndio ukweli

Mohamed, mmoja kati ya vijana weledi wa taifa letu, mjenzi na mtetezi wa hoja bila kutetereka. Daa!

Poleni ndugu jamaa na marafiki, na wananchi wote

Sisi sote ni wa mola na kwake tutarejea. R.I.P Mohamed
 
Duniani tunapita binadamu kama maua huchanua asubuhi na jioni hunyauka,
tukubali kumpokea YESU kujiandaa kwa maisha yajayo.

Pumuzika kamanda mtoi wote tuko njiani.
 
Jaman kwanini lakini, Kijana muhimu, mdogo anatuacha wakati wanajamii tukisubiria kuona tukiongozwa naye??? May you're soul rest in peace brother.
 
Dah!!

Habari za kusikitisha sana hizi...
 
Tangu nimepata hizi taarifa naona hata ubongo unakataa...najihisi nipo ndotoni na nikiamka itakuwa tofauti
 
Back
Top Bottom