TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

Mungu akurehemu rafiki yangu mpendwa... Wote tupo njia hoyo kaka Mohamedi Mtoi. Hatujui nani anafuata. Maisha haya ni mafupi, na wote tupo hapa ni mavuno ya Mungu wetu.
Nazidi kumwomba Mungu aipe familia nguvu na ustahimilivu wakati huu mgumu wa majonzi.
 
Tangulia kamanda, sie wote ni wake Mola na kwake ni marejeo
 
R.I.P Mtoi.

Fundisho tuliobaki: Tusikubali kuitika ulaghai wa Mbowe na Lowassa ili yakitukuta tuwe na amani.
 
RIP Mohamed Mtoi tunaomba Mungu ailinde familia yako iliyobaki na aipe Amani yake
AMEEN
 
So sad jamani! Tukiwa bado tunaendelea na maombolezo na kwa kuwa maisha ni lazima yaendelee, vipi kuhusu nafasi yake aliyokuwa anagombea? Ndio ccm wamepita bila kupingwa au CDM inaweza weka mgombea mwingine? Sheria inasemaje hapa?
 
Jamii forums anzisheni mfuko maalum wa rambirambi kwa ajili ya familia ameacha watoto wadogo sana
 
Dah, pigo. Jamaa alikuwa ananielewa sehemu nyingine nilipokuwa mgumu kueleweka na wengi.

May all beings attain enlightenment.

..umesema kweli kabisa.

..yaani huyu dogo alikuwa kijana mtulivu ktk mijadala, na tena msikivu. nilimpenda kama mdogo wangu.

..kila nikimtumia ujumbe alikuwa mwepesi kujibu. ukimuuliza maswali mwepesi kuyajibu. tukimrushia maduku-duku yetu kuhusu chadema hakusita kutujibu tena kwa uungwana wa hali ya juu.

..lakini nisichokisahau ni kila ujumbe wake alionitumia, alimaliza na maneno, KILA JEMA NA LENYE KHERI LISIKUPONYOKE.



cc Nguruvi3, lusungo, Jasusi
 
Last edited by a moderator:
RIP Kamanda Mohamed Mtoi,
Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.
Poleni wote tulioguswa na Msiba huu, tena wakati huu wa Uchaguzi.


Taarifa za hivi punde nikuwa kamanda Mohamedi Mtoi amepata ajali na kufariki dunia

WAMETOKA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI TARAFA YA MLOLA.
KAMANDA MTOI AKAWAPELEKA WENZAKE MPAKA LUSHOTO MJINI KISHA AKAONDOKA KUELEKEA NYUMBANI KWAKE NDIO NJIANI GARI IKAPATA AJALI NA NDIPO KAMANDA MTOI AKAFARIKI DUNIA.

Maelezo haya yamethibitishwa na katibu wa chama wilaya Lushoto Kamanda Dulla.

========
UPDATES:
 
RIP Mohamed. Ulale pema peponi. Tutaendeleza mapambano kukuenzi. Sad.
 
Só sad nimeumia sana! Muasisi wa mabadiliko aliyekosa kuona mabadiliko uliyo yapigania miaka mingi
Pumzika kwa Amani kaka mtoi
 
Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.. so Sad... kazi yake haina makosa
 
My condolence to the family and the people of Lushoto, Mungu awape matumaini na faraja wapendwa wote
 
Back
Top Bottom