TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

Lala Pema mwanamapinduzi damu yako haitapotea bure, tutashinda dhuluma na uonevu wa CCM na wapigania matumbo Yao. Amen
 
Amefariki kwa ajali inasemekana alikuwa na mwanamziki Roma Mkatoliki

chanzo cm toka muheza ila sina uhakika

kama ni kweli basi familia ya mzee Mtoi inabahati mbaya sana kwani mdogo wa Mohamedi mtoi alifariki pia kwenye tukio la mabomu kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha.

Muhamedi Mtoi ni mwanaharakati wa muda mrefu wa CHADEMA. Amekuwa akishiriki harakati nyinga za kujenga chadema mkoani Arusha na Tanga pia ni Moja kati ya wanajamii Forum anayepost habari nyingi kuhusu harakati za chadema na hana chembe ya uoga kwani hutumia jina lake halisi Mohamed Mtoi

___=_____________________
huu ni uzi ulionifanya nimfatilie na kumfahanu vizuri Mohamedi Mtoi

Topic: Kijana Amiri Mtoi mhanga wa
bomu la Arusha amezikwa leo Mkuzi -
Lushoto.
Page 14 of 14 First ... 4 12 13 14
Mohamedi Mtoi 17:24 19th June 2013
Ndugu zangu.
Kijana Amiri Mtoi ambaye ni mtoto wa
kaka yetu Mtoi Kolowa Daffa (mtoto wa
baba yetu mkubwa) amezikwa leo
majira ya saa 5 kijijini kwetu Mkuzi
wilayani Lushoto.
Marehemu Amiri ni miongoni mwa
wahanga wa tukio la bomu kule Arusha,
amesafirishwa usiku kuamkia leo na
amezikwa mapema asubuhi kufuatia
imani ya dini yetu lakini pia ili kutoa
fursa ya watu walio sindikiza mwili
kutoka Arusha waianze safari yao
mapema.
Amiri Mtoi amekatishwa masomo
angali darasa la tatu, amiri hakuwahi
kufikiri wala kuzadhani kuwa atakufa
akiwa na tundu la risasi kwenye mwili
wake, nimeangalia picha zake
nimeumia sana, ametangulia mbele ya
haki, walio rusha risasi nao
watamfuata, Mwenyezi Mungu
atawalipa, sio kwa dua mbaya za
familia, lakini kwa mapenzi yake yeye
(Mungu).
Watu wa Arusha kwa wingi na umoja
wao wameonyesha ushirikiano wa
kutosha.
Kwa niaba ya wana ukoo wa Mtoi
tunawashukuru sana!
Tumuombee Amiri apumzike kwa amani
baada ya kukatishwa uhai wake na
watu wasio kuwa na huruma na wenye
kujiona wao pekee ndio wenye mamlaka
ya kuitawala Tanzania na kuamua nani
aishi na nani atangulie mbele za
Mungu.
Itoshe kusema.
Inauma sana, hasira zangu dhidi ya
ccm hazita koma na wamefungua
ukurasa mpya wa mapambano dhidi
yao, sisi ni maskini na wanyonge
hatuwezi kumiliki bunduki wala bastola
zenye risasi lakini tunaweza kuuwa kwa
kutumia sanduku la kura. Nitayaongoza
mapambano
"All those that fight when oppressed
incur no guilt, but Allah shall punish the
oppressor." Come the day.
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un
Sent from my BlackBerry 9860 using
JamiiForums.
 
Ni nani aijuae kesho? Tumepoteza mpiganaji wa kweli, Ulale salama peponi MM.
 
Naam, vijana wa Lumumba wale waliokuwa wanaeneza propaganda chafu za udini dhidi ya cdm watakua wanamkumbuka huyu kamanda.

Nimeumia sn.......RIP kamanda kwa Mara ingine tena!

Acha kuchafua hali ya hewa hapa. Peleka bangi zako mbele huko. Ndio maana tunawaita Baraza la vichaa chadema. Hapa watu wanazungumza mambo ya msiba,na yoyote atakayeondoka nje ya mada ya msiba ni mwehu. Inna lillah waina ilayhi rajiuun. Mwenyeezi Mungu amsamehe madhambi yake amtayarishie makazi mema huko endako
 
Daaaah!!, inauma sanaaa. Mungu na awe pamoja na wafiwa wote
 
Kwa kweli Hii ni habàri mbaya sana . Na kimsingi siku yangu imeanza vibaya kuliko kawaida. R.I.P kamanda
 
Kijana Lowassa hadhihakiwi ni mgonjwa kweli.

Hapana, nisingempa kura yangu hata kama angegombea CCM

Sababu kubwa sana na ya muhimu ya kutokumchaguwa Lowassa na napenda kuwatanabahisha Watanzania kutomchaguwa ni la ugonjwa alionao, dhambi binadam anaweza kutubu, lakini hili la maradhi ni kubwa sana jisomee tatizo la ma-mvi:

AlhamduliLlah, mie mzima wa afya tele.

Ninakuombea na wewe uzima na afya.

Lowassa hali yake kiafya haimruhusu kabisa kuongoza hata nyumba kumi, wacha nchi.

Tuwache ushabiki wa kijinga, tunaongelea mtu anaetakiwa kuongoza watu zaidi ya million 45.

Isitoshe, kuna kuumwa magonjwa ambayo yanajulikana kabisa kuwa haya hayana madhara na hayahusishi uelewa na ufahamu wake, yanatibika na ya kupita tu, lakini kwa Lowassa, hebu jisomee hapa chini:

Medical diagnosis
Parkinson's often starts with a tremor in one hand. Other symptoms are slow movement, stiffness, and loss of balance.
People may experience:

Tremor:
can be postural, can occur at rest, in the hands, or limbs

Muscular:
difficulty standing, difficulty walking, difficulty with bodily movement, involuntary movements, muscle rigidity, muscle twitch, problems with coordination, slow bodily movement, stiff muscles, or slow shuffling gait

Cognitive:
amnesia, confusion in the evening hours, dementia, or difficulty thinking and understanding

Sleep:
daytime sleepiness, early awakening, nightmares, restless sleep, or sleep disturbances

Sensory:
distorted sense of smell, loss in contrast sensitivity, or loss of smell

Speech:
impaired voice, soft speech, or voice box spasms

Facial:
jaw stiffness or reduced facial expression

Urinary:
dribbling of urine or leaking of urine

Whole body:
dizziness, fatigue, or poor balance

Psychological:
anxiety or depression

Also common:
apathy, blank stare, constipation, difficulty swallowing, drooling, falling, fear of falling, neck tightness, restlessness, small handwriting, trembling, unintentional writhing, or weight loss

Bado tu tumpe Urais mtu namna hiyo? No. No. No.

Ukimchaguwa mtu mwenye ugonjwa kama wa Lowassa itakuwa hujitendei haki wewe mwenyewe na watoto zetu ambao hawajafikia umri wa kupiga kura - Kumbuka hilo.

Halafu wananishangaza zaidi CUF, kauli mbiu yao ni "haki sawa kwa wote" sasa kumchaguwa mgonjwa ni kutenda haki sawa kwa wote? - Wanazidhulumu nafsi zao na wale wanaowatagemea kuwa watafanya maumuzi sahihi, hususan watoto ambao hawajafikia umri wa kupiga kura.

toa uharo wako hapa.
 
Acha kuchafua hali ya hewa hapa. Peleka bangi zako mbele huko. Ndio maana tunawaita Baraza la vichaa chadema. Hapa watu wanazungumza mambo ya msiba,na yoyote atakayeondoka nje ya mada ya msiba ni mwehu. Inna lillah waina ilayhi rajiuun. Mwenyeezi Mungu amsamehe madhambi yake amtayarishie makazi mema huko endako

We mwehu nini..... Toa upuuzi wako hapa...
 
Daaah what a bad way to start a sunday.... RIP kamanda Mtoi, tunakuhakikishia kuendeleza mapambano mpaka kieleweke
 
Hii taarifa sio nzuri kwa kweli. Nimepigia jamaa yangu yupo Lushoto nimemuulizia kuhusu mazingira ya kifo cha Mtoi, jamaa amestuka sana akakaa kimya kwa muda na kilichofuata nimesikia kilio na simu imekatwa.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA KAMANDA WETU.
 
Back
Top Bottom