TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

It is reported that the Prophet :swalalahu alaihi wasallam has said:

Whosoever covers (the sins of) a Muslim, Allah will covers (his sins) on the Day of Judgment. (Reported by Bukhari)

If we find it too difficult to keep it secret, the most we are allowed to do is discuss the issue with the person, in private, and try to encourage them to stop committing the sin(s).

Allah has said:

The believers, men and women, are Auliyâ' (helpers, supporters, friends, protectors) of one another, they enjoin Al-Ma'rûf (i.e. Islâmic Monotheism and all that Islâm orders one to do), and they forbid (people) from Al-Munkar (i.e. polytheism and disbelief of all kinds, and all that Islâm has forbidden). (Quran, 71:9)

Ulikuwa unataka kumaanisha nini mkuu.
 
AYUBU 14:1-2

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa!. Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.

-------------------------------------
-------------------------------------
AYUBU 14: 6-7
Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita:
Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika, Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.

Kwani yako matumaini ya mti ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma.
----------------------------------------

Umetufariji sana mkuu
 
Wakuu poleni na mapuziko wakati huo huo napenda nitoe pole zangu kwa wanafamilia wote wa JF kwa kumpoteza mwana JF mwenzetu ndugu yetu Mohamed Mtoi ni habari mbaya kiukweli si habari nzuri kwa wote wapenda mabadiliko hata kwa wale wasiopenda mabadiliko...baada ya kupata taarifa ya msiba wa huyu mpendwa wetu nimeumia sana kiukweli sio siri ukanikumbusha msiba wa dada yangu Regia Mtema....niseme wazi sijawahi kukutana na huyu mtu wala kuongea naye sehemu yoyote ile zaidi ya kumsoma humu ndani vile vile kwa dada Regia mtema lakini cha kushangza JF inafanya hawa watu kama nimeshawahi kuonana nao vile na kushi nao sana tu....hata pale members wengine wanavyopata matatizo mengine na kuyaandika humu haswa yale ya kusikitisha sana unajikuta unaguswa sana na kuumia kama vile huyo mtu uliwahi kuonana naye zaidi ya maandishi yake ya humu ndani...Nilichojifunza tokana na msiba wa kaka mtoi humu ndani kumbe tunahitaji kuvumiliana sana na kudumisha upendo kama wana JF.....Japo kuna people zinakera sana lakini no way tunahitaji upendo,kuvumiliana na kupaena nguvu kila tunapopata vikwazo...japo wengi ni ID fake lakini hii JF inatuunganisha sana na haifichi uhalisia wa mioyo yetu...Mwenyezi Mungu Mwingi wa Huruma na Rehema amlaze ndugu yetu Mohamed Mtoi na wanafamilia wengine walio tutangulia mbele ya haki mahala pema peponi.
 
Lala salama Mtoi, JF members tutakumiss sana!

[video]https://youtu.be/NoOhnrjdYOc[/video]
 
Nenda kapumzike kamanda.Damu yako italikomboa taifa October
 
R.I.P kamanda Mtoi,mchango wako tutaukumbuka sana katika mapambano ya ukombozi dhidi ya nduli ccm.

Mambo ya nduli yanatoka wapi sasa! mweche mwenzio akaangalie mavuno yake kwa Allah bana! Inna lilah, wainnailaih rajiun.
 
Kuna member ameandika watu wema hawadumu.Ningeweza muuliza MUNGU ningemwambia "Mbona umemchukua mapema namna hii?? Lakini nimeumia na kusikitika sana juu ya ndugu Mohammed..Apumzike kwa amani na MUNGU amwangazie nuru ya milele.
 
Apumzike kwa Amani Kamanda Mohamed Mtoi.
Tumepoteza, tusonge mbele na MABADILIKO 2015. R.I.P
 
Nimestushwa sana na kusikitishwa na kifo cha Mohamedi Mtoi Kanyawana, kilichotokea kwa ajali usiku wa kuamkia leo akiwa katika harakati za kampeni. Ni miongoni mwa vijana ambao waliamini hasa katika mabadiliko ya kweli na walikitumikia chama chake kwa kadiri ya uwezo wake. Mungu ailaze roho yake pema peponi, na kuwapa faraja familia yake, ndugu, wanachadema na marafiki wote ambao wameguswa na msiba huu. Ameen
 
Mtoi nitakukumbuka sana! Kuna siku ulinishauri kuachana na CCM, Nikakutukana! Ila sasa hivi nakumbuka sana maneno yako! Ila ninachoshukuru Mungu hivi sasa siko tena CCM.

Lala salama MTOI, umetangulia mbele ya haki, ila maono yako yataishi milele!

Wakristo tunaaamini kuwa baada ya maisha haya ya duniani kuna maisha mengine, ambayo yatatukutanisha sote!

Naamini tutakutana tena baada ya maisha yetu hapa Jamii forums!

[h=1]Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un[/h]
 
What a waste dying at such a young and promising age! RIP Mohamed Mtoi.
 
Innalilaah Waina Ilayhi Rajiun - Kwake Mola ndiko tulikotoka na kwake tutarejea. Mwenyezi Mungu akupe kauli thabit..
 
Back
Top Bottom