Mwanachama wa Yanga Mwigulu Nchema amrudisha Kocha Pluijm

Mwanachama wa Yanga Mwigulu Nchema amrudisha Kocha Pluijm

Moja ya kazi ya waziri wa mambo ya ndani ni kutatua migogoro katika jamii.
 
Mh.Mwigulu angehangaika Na Panya Road Na Majambazi kuliko Yanga , Yanga amwachie Waziri mwenye dhamana Na Michezo mkuu
Usikariri maisha na kuishi kama Kasuku, tenganisha Taaluma/Kazi na Hobby! Juha Kalulu weee!
 
Wadau naomba mnijuze hivi Mh.Mwigulu Mchemba ni Waziri wa Michezo au Mambo ya ndani?Nasema hivyo kutokanabna kujikita kwenye masuala ya Klabu ya Yanga zaidi.Anayejua anifahamishe.
Sasa atafanya kazi gani bana?wakati magufuli anaongoza na kuingilia kila kitu muache azame kwenye michezo.hapo namtetea mwigulu hapo.
 
Wadau naomba mnijuze hivi Mh.Mwigulu Mchemba ni Waziri wa Michezo au Mambo ya ndani?Nasema hivyo kutokanabna kujikita kwenye masuala ya Klabu ya Yanga zaidi.Anayejua anifahamishe.


Mimi sioni Tatizo lolote,
Mwigulu ni Mshabiki na Mdau na Mnazi wa Yanga.
Migogoro mingi kwenye Timu zetu, zinadidimisha Soka letu.
 
Hata Mbowe angehusika kumrejesha wote ni Yanga damu hao
Ndugu yangu akili za kuvukia barabara watu wanataka wafanyie biashara ni vitu viwili tofauti mwigulu au mbowe kama ulivyoandika wangefanya kama wana jangwani sio kila kitu watu walete siasa za tope.
 
Wabongo na nyie mmezidi kila kitu kukosoa tu mda mwingine mjiongeze kwani mtu akiwa waziri wa ndani ndo kazuiwa kufatilia michezo?
 
Wanauwe wa dar acheni kutusumbua na vipanya road vyenu,wanauwe wazima mnashindwa kuanzisha hata vikundi vya sungu sungu kazi yenu kushinda club tu
 
Kaaz kwel kwel..saiv kuna uwezekano huyo kocha akaboronga halaf wadau wakaogopa kumpiga chini mana waziri anaweza kurudi na mamlaka
 
Jamaa povu linawatoka kisa mwigulu km waziri kutumia ushawishi wake kuweka mambo sawa pale Yanga,kisa tuu ye yupo Simba basi mishipa imemsimama,nyoo kwani Yanga ipo nchi gani? Km ye waziri wa mambo ya ndani na humo ndani Yanga pia Imoooooo..


Kalambe ndimu km hupendi..
 
siasa zaingia rasmi uwanjani ......twendeni tu
Lakini hii imenisaidia mimi kubadili mtizamo wangu, kwa baadhi ya viongozi wa serikali, Ujambazi na uharifu kijumla umeongezeka waziri sijawahi kumsikia akiongea chochote, ila yuko bize na mambo ya Yanga, anafaa kuwa kiongozi Yanga, ila nimshukuru waziri kwa kunifanya nibadili mtizamo kwa baadhi ya viongozi wetu.
 
Huyu kocha hana tofauti na lipumba mwendo wa kukanusha...
 
Back
Top Bottom