Kama unataka "aftatu" tu kwa siku mbona simple. Hiyo ni kama $1 kwa siku. Ingia SproutGigs zamani walikuwa wanaiita Picoworkers au site yoyote ya micro-jobs kupata $1 ni suala la dakika tu.
Zamani nilikuwa naitumia kwa siku saa 1 tu. Nilikuwa nafanya tasks za ku-like posts za Reddit tu kwa malipo ya $0.03 kwa kazi, ni dakika tu una-like unapewa chako. Kwa siku nilikuwa napiga tasks 50. Hiyo ni $10 (easy money) kwa wiki. Zipo kazi zinazolipa zaidi ni wewe tu na muda wako.
Mtaji ni smartphone yako, bando na muda mchache tu, hutumii nguvu nyingi. Tangu walipobadilisha kuwa SproutGigs sijaitumia, hizo kazi zinafaa kwa wale wasio na mishe ya kufanya kabisa. $10 kwa wiki ni nyingi kwasababu bado ni mwanachuo.
Njia za malipo ni rahisi tu, mimi nilikuwa natoa kupitia Skrill kwenda 1xBet halafu natoa kwa wakala wa 1xBet. Ukitoa usiku, asubuhi unakutana na email ya maokoto kwenye Skrill yako.