Mwanachuo UDOM jela miaka 6

Afyayaakili

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2012
Posts
924
Reaction score
1,263
Mwanachuo Udom jela miaka sita
By Hadija Jumanne, Mwananchi

Imewekwa Friday, September 26 2014 at 09:45

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka sita jela, Melkiad Kabunduguru(28) baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kukutwa na noti bandia.

Kabunduguru ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma(Udom) atatumikia kifungo hicho baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa dhidi yake.

Katika shtaka la kwanza la Kabunduguru atatumikia kifungo cha miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu huku shtaka la pili la kukutwa na noti 50 za bandia za Sh5000 mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Juma Hassani alisema mshtakiwa atatumikia vifungo hivyo kwa pamoja baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Juma Hassani alidai kuwa mshtakiwa huyo atatumikia kifungo hicho ili iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia za wizi.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha mashtaka, Felista Mosha uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia za udanganyifu.
 
Safi iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.
 
Dah inamana jamaa hapewi hata muda wa kumalizia chuo?
 
Safi iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Fundisho wapi mbona wakina Riz1 na madawa ya kulevya lakini ndo mnawapa na ubunge kama reward kwanini nao wasifungwe ili iwe fundisho? Au watoto wa maskini ndio huwa sample.. Agrrrrh
 
Nachukia sana matapeli. Fikiria una duka unauza vocha umemuacha kijana wajanja wanampa noti bandia kama za 50,000.
 
Kwahyo hapo atawekwa jela kwa mda wa miezi 32 sawa na miaka miwili na miezi 8.
 
Safi iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Fundisho kwa masikini pekee. Majizi serikalini no fundisho ni ruksa kuiba. Usikute wamesingiziwa kwa sababu ya siasa. Na kama nchi inafuata sheria mbona inakomoa raia wake hii hawa mahakimu wa picchu ni janga pia la taifa
 
Fundisho wapi mbona wakina Riz1 na madawa ya kulevya lakini ndo mnawapa na ubunge kama reward kwanini nao wasifungwe ili iwe fundisho? Au watoto wa maskini ndio huwa sample.. Agrrrrh

Mmh siku zote maskin ndio anaye fungwa jela
 
Watu wanapenda maisha ya bure mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…