Tegry,
Mbuzi alizaliwa na mbuzi aliyezaliwa na mbuzi.
Analogue: Siku moja nilipita sehemu nikakuta tangazo limebandikwa ukutani linasomeka hivi: "USIPOJIANDIKISHA HUTAPIGA KURA".Kwenye tangazo hilo alikuja mtu fulani na kalamu halafu akaandika kwenye karatasi hiyo hiyo, mbele ya hayo maandishi akauliza swali linasema hivi "USIPOPIGA KURA JE?", Baadaye tena alikuja mtu wa pili akakuta hilo swali lililokuwa limeulizwa halafu naye bahati nzuri akapata nafasi ya kulijibu akaandika hivi "HUTAJIANDIKISHA", nadhani umepata mlolongo huo.
Kwa hiyo tutumie logic hiyo ili kuweza kujua kuwa mbuzi alitoka wapi, kwamba kama usipojiandikisha huwezi kupiga kura ina maana usipopiga kura hutajiandikisha! Vivyo hivyo kama mtu ni mtoto wa mtu aliyezaliwa na mtu, basi mbuzi naye ni mtoto wa mbuzi,aliyezaliwa na mbuzi!