kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,779
- 4,982
Katika pita pita zangu, nimekutana na hoja ya pasta mmoja wa Kenya akisema kuwa kuna Mungu na pia kuna miungu, na miungu ni sisi wanadamu. Watu walicheka sana na kumuita mnafiki.
Kuna watu wengi wanashindwa kuelewa maana ya neno Mungu. Wanafikiri Mungu (Allah) ni jina la Yehova au Yahweh. Neno Mungu lina maana nyingi sana, lakini maana yake kuu ni "mwenye uwezo." Pia, neno Mungu lina asili kama lilivyo neno mwanadamu. Neno Mungu linarejelea yule aliye juu ya yote.
Swali langu rahisi likawa, kama mtu kwa kufanyika mwanadamu anachukua asili ya kibinadamu (anaitwa mwanadamu), je, mtu kwa kufanyika Mungu aitwe nani? Na achukue asili ya nani?
Hoja yangu siyo hiyo; hoja yangu ni kwamba mwanadamu anastahili kuitwa Mungu. Tukienda katika maandiko matakatifu, Yesu alimuita Shetani "Mungu wa dunia." Kwanini? Kwasababu ya uwezo na nguvu za Shetani, ndiyo maana anaitwa Mungu wa dunia. Je, Yesu alikufuru? Hapana.
Kwanini basi mwanadamu mwenye uwezo naye asiitwe Mungu?