"Mwanadamu wa kawaida" huwezi kuelewa

"Mwanadamu wa kawaida" huwezi kuelewa

Mara nyingi nimekua nikiona watu wanaoleta mada ambazo wanadhani ni ngumu kueleweka (hasa jukwaa hili) hua wanapenda kutumia misemo kama "Kwa akili ya kawaida huwezi kuelewa" au "mtu wa kawaida hatanielewa" au utasikia "swala hili liko nje ya upeo wa akili za mwanadamu" (hasa mambo ya dini) n.k.

Mimi siku zote nimekua nikijiuliza "kama swala liko nje ya upeo wa akili ya mwanadamu, au haliwezi kueleweka kwa akili ya mwanadamu, huyo anaeliwasilisha yeye hua ametumia akili ya wapi kuweza kulielewa?"

Chief ngoja nikupe ufafanuzi juu ya kauli hii au kauli hizo.

Katika kuwasilisha mambo lugha huwa jambo la msingi sana. Lugha imegawanyika katika sehemu kuu mbili,kuna lugha ya kifani na lugha ya kawaida ya mazungumzo tunayo zungumza,mathalani leo hii huwezi kutumia lugha ya kifasihi ya ndani kwa mwananchi anae hitaji lugha nyepesi sana. Haoa watu wa fasihi huwa wanasema mtu lazima uzungumze jambo kulingana na hadhira ikoje.

Sasa swali la msingi ni wakati gani jambo huwa gumu kueleweka ? Kabla ya hapo,akili ya mwanadamu iko tayari kupokea chochote endapo kikiwekwa katika hali nyepesi na kueleweka.

Sababu za mada au jambo kutokueleweka.
1. Lugha,hii ni sababu ya msingi sana ambayo wawasilishaji wa mada wanatakiwa kulizingatia,yaani muwasilishaji mada anatakiwa aangalie mahitaji ya hadhira.

2. Ufasaha wa muwasilishaji,hili pia ni jambo la msingi. Wawasilishaji wametofautiana vipawa na namna ya uwasilishaji jambo,hili si jambo geni. Leo unaweza kuelezewa maana ya "Elimu" na msomi fulani usielewe na ukaelezewa maana ya "Elimu" na msomi mwingine ukaelewa na wala usihitaji kupewa mifano.

3. Umakini wa msikilizaji,kuna watu wengine huwa wakielezewa jambo wao wanafanya mengine na mfano wake,huwa tunasema hivi mshika mawili moja hushika njia.

4. Kutokuwa na ufahamu wa jambo linalowasilishwa. Hapa inaingia kwa muwasilishaji na hadhira.

Angalizo : Akili ya mwandamu ni hii hii ambayo wewe ubayo na mimi ninayo,tofauti zetu ni katika juhudi na kufikiria sana,yaani matumizi ya akili.

Nipo ....
 
Okay..Nimekusoma mkuu.
Ila TL mbona ni mtu mwenye kusaidia sana wanyonge.
Sema huwa hafichi ukwel ndio kitu kinachofanya wenmgine wamtafsiri kama mtu mwenye majivuno.
Sema

Mimi sijasema ni mtu mwenye majivuno, bali nimeongelea UFO kwa war akili ni vitu viwili tofauti.
 
Mimi nafikiri tukubaliane kwamba binadamu wote tuna akili za kawaida. Labda tofauti inakuja pale ambapo mtu umeamua kuinoa akili yako kwenye eneo fulani kwahiyo unakua unajua zaidi kuhusu eneo hilo, ila sio kwamba una akili isiyo ya kawaida.
 
Mara nyingi nimekua nikiona watu wanaoleta mada ambazo wanadhani ni ngumu kueleweka (hasa jukwaa hili) hua wanapenda kutumia misemo kama "Kwa akili ya kawaida huwezi kuelewa" au "mtu wa kawaida hatanielewa" au utasikia "swala hili liko nje ya upeo wa akili za mwanadamu" (hasa mambo ya dini) n.k.

Mimi siku zote nimekua nikijiuliza "kama swala liko nje ya upeo wa akili ya mwanadamu, au haliwezi kueleweka kwa akili ya mwanadamu, huyo anaeliwasilisha yeye hua ametumia akili ya wapi kuweza kulielewa?"

conscious mind
 
Wanasema mungu achunguziki kwa akili yako ya kawaida, mara biblia na kuraan havisomwi kama gazeti why?,,,,, This is bullshit

Hata mimi komenti yangu huwezi ukasoma ukaelewa kwa akili yako ya kawaida

Sent using unknown device
 
Mara nyingi nimekua nikiona watu wanaoleta mada ambazo wanadhani ni ngumu kueleweka (hasa jukwaa hili) hua wanapenda kutumia misemo kama "Kwa akili ya kawaida huwezi kuelewa" au "mtu wa kawaida hatanielewa" au utasikia "swala hili liko nje ya upeo wa akili za mwanadamu" (hasa mambo ya dini) n.k.

Mimi siku zote nimekua nikijiuliza "kama swala liko nje ya upeo wa akili ya mwanadamu, au haliwezi kueleweka kwa akili ya mwanadamu, huyo anaeliwasilisha yeye hua ametumia akili ya wapi kuweza kulielewa?"
Anakuwa ameshushiwa na roho mtakatifu, 'tifu' mtaani kwetu maana yake fujo, kwa hiyo nikisema " anakuwa ameshushiwa na roho mtakafujo" mnisamehe bure!
 
Sasa mkuu mtu anapoleta mada na anaweka kabisa angalizo kwamba kitu hiki kwa akili ya binadamu wa kawaida hamuwezi kuelewa, wakati binadamu wote tuna tumia akili hii hii ya binadamu, anakua ana maana gani?
Mambo mengine ni mbwembwe na tambo tu za humu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nilikuwa nadhani ile akili isiyokuwa ya kawaida ni akili ya KICHAA. Mwanadamu asiye wa kawaida mi nilikuwa najua labda ni MSUKULE. Nashukuru kwa ufafanuzi umenitoa giza mtoa mada.
 
Naunga mkono hoja
Hizi kauli zinachefua sana. Hata kama ndio hautaeleweka basi tueleweshe,hii tabia ya watu fulani kujiona Extraordinary inachefua sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Human being is rational being, ni kiumbe ambae anauwezi wa kufikiria kwasababu an hiyo hali kichwani kwake, hakuna binadamu wa kawaida na binadamu special kwa kuwa wote wana hiyo reasoning ability, tunatofautiana kwenye matumizi tu ya huo uwezo kuna wengine wanatumia asilimia 10, 20, 30..... na hakuna mipaka kwenye matumizi ni namna tu unavyoji condion mwenyewe. Mfano kutoka ama kubakia kwenye unnecessary comfortability zone, ku deal na simple things badala na complicated matters, to discuss people aka ubuyu badala ya ideas and other matters related to them.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jitahidi kusoma vitabu, makala mbali mbali ili kupanua ufahamu wako. Mfano tunaamini kwamba sisi ndio binadamu wa kwanza kuishi hapa duniani. Lkn ukiwa mdadisi na kusoma vitabu na makala mbali mbali utakuja gundua kwamba kabla yetu kulikuwa na jamii iliyoendelea sana ilikwepo kabla yetu. Ndio hao waliojenga majumba makubwa makubwa ambayo tofali lake moja ni km behewa la treni. Hii jamii ya watu wakubwa Giants ilikuja teketetezwa wakati wa great floods au Gharika kuu. Nenda Mexico, Misri, Lebanon Syria, Iraq, India Japan utakuta hizo Megalithic structures zilizobakia.
Kwenye haya majengo utakuta picha zimechorwa za astronauts wa kale na ndiyo tecnolojia wana anga wa sasa wanatumia. Hayo majengo yalijengwa kwa mawe na si tofali km zetu hizi. Jiwe limekatwa vizuri kama wewe unavyoweza chonga kinyago cha mbao. Jiwe kubwa kama behewa la treni limetobolewa katikati, na kuchongwa vizuri. Technolojia hiyo bado hatuna.
Kwa hiyo kwa akili ya kukaririshwa tu vitabu vyetu hivi huwezi fikiria nje ya box
Tuseme ukweli hapa mkuu unatumia akili usiyo ya kawaida kutuburuza wenye akili za kawaida!
 
Tuseme ukweli hapa mkuu unatumia akili usiyo ya kawaida kutuburuza wenye akili za kawaida!
Jionee mwenyewe hizo Megalithic structures. Hakuna mashine inayoweza nyanyua Hilo jiwe kwa teknolojia yetu sasa. Ni mawe makubwa yamekatwa yakakatika. Niambie wapi sasa hivi unaweza kuta wamekata mawe makubwa kama hayo
FB_IMG_1549863071676.jpg
FB_IMG_1549863003051.jpg
FB_IMG_1549862992152.jpg
 
Mara nyingi nimekua nikiona watu wanaoleta mada ambazo wanadhani ni ngumu kueleweka (hasa jukwaa hili) hua wanapenda kutumia misemo kama "Kwa akili ya kawaida huwezi kuelewa" au "mtu wa kawaida hatanielewa" au utasikia "swala hili liko nje ya upeo wa akili za mwanadamu" (hasa mambo ya dini) n.k.

Mimi siku zote nimekua nikijiuliza "kama swala liko nje ya upeo wa akili ya mwanadamu, au haliwezi kueleweka kwa akili ya mwanadamu, huyo anaeliwasilisha yeye hua ametumia akili ya wapi kuweza kulielewa?"

Nguvu za kiroho

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna wanaotaka kujua mambo kwa kutumia akili badala ya kutumia akili kuelewa mambo,hawa ndio wanaojiona wana akili zaidi ya wenzao na kuwaona watu wa dini hawatumii akili.
Lakini pia kuna watu wa dini wanatumia hisia kuelewa mambo badala ya akili na ndiyo husema huwezi kuelewa kwa akili ya binaadamu,mfano kama utatu au roho,hakuna mwenye kuvielewa hivyo vitu na ndiyo hapo sasa mtu akishindwa kuelezea anakimbilia kusema huwezi kuelewa kwa akili ya kawaida hivyo ni wazi yeye anatumia hisia kuelewa na si akili.
 
Back
Top Bottom