Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Ni ke au me?Lasmini Kondo mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Masaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani, amekutwa akiwa amejinyonga baada ya kukatazwa na wazazi wake kutojihusisha na mapenzi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani, ACP Pius Lututumo amesema mwanafunzi huyo amejinyonga baada ya kugombezwa na wazazi wake kutojihusisha na mapenzi kufuatia kukutwa na barua aliyokuwa amemuandikia mpenzi wake.
“Baada ya wazazi wake kukuta barua ambayo marehemu alimuandikia mpenzi wake walimfokea kwa kumtaka kuachana na masuala hayo kwani yeye ni mwanafuzi.
“Kutokana na kitendo hicho marehemu aliamua kuchukua uamuzi wa kujinyonga jambo ambalo linasikitisha,” amesema.
Jamhuri
Hujafafanua.