The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kagemu iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Caren Mwemezi (18) amekutwa amejinyonga nyumbani kwao mtaa wa Nyakanyasi huku sababu zikitajwa kuwa ni kulazimishwa kuhudhuria masomo na kukatazwa kucheza michezo ya kubahatisha (bonanza)
Akizungumzia tukio hilo mama mzazi wa Kijana huyo Rosemary Fadhiri amesema kuwa kijana huyo enzi za uhai wake alikuwa akitumia muda wa masomo kwenda na wenzake kucheza michezo ya kubahatisha
"Alikuwa anasomea shule ya sekondari Kagemu lakini alikuwa na anachangamoto ya kutoroka mara muda mwingine haendi anacheza bonanza, nilikuwa nafatilia shuleni naenda na leo nilikuwa nafatilia nimefika hadi kwa Mwenyekiti asubuhi kumtafuta narudi naambiwa Caren amejinyonga" amesema Mama mzazi wa Caren.