Mwanafunzi aliyemaliza darasa la 7 ajinyonga baada ya kukatazwa na Mama yake asirudi nyumbani usiku

Mwanafunzi aliyemaliza darasa la 7 ajinyonga baada ya kukatazwa na Mama yake asirudi nyumbani usiku

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwanafunzi aliyemaliza darasa la 7 wiki iliyopita katika shule ya msingi Njungwa, Kijiji cha Ngayaki wilayani Gairo, Rahel Yohana (14), amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kanga huku chanzo kikitajwa ni ugomvi kati yake na mama yake mzazi aliyekuwa akimkataza kurudi nyumbani usiku.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 15 mwaka huu, na akatoa wito kwa wale watu wanaoona njia ya bora ya kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kukatisha uhai wao, kuwa siyo sahihi na badala yake watafute ufumbuzi wa changamoto zao kwa wataalam.

"Aligombezwa na Mama yake kwa kosa la kurudi nyumbani mara kwa mara usiku na alitoweka nyumbani na ndipo alipokutwa amejinyoga vichakani, nitoe wito kwa watu ambao wanafikiri 'shortcuts' ya changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kuamua kujinyonga, hiyo si sahihi ni bora ukutane na wataalam wa kisaikolojia ili wakusaidie", amesema Kamanda Mutafungwa.

Na mwili wa mtoto huyo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.
 
Dogo hapendi kupangiwa, ameamua aondoke nyumbani milele.
 
Mtoto mjinga sana, heri kajitoa mwenyewe uhai maana huko duniani yangemkuta mengi.
Asiyefundishwa na mamaye hufundishwa na dunia.
 
Pole sana kwa mama mzazi. Alikua anajitahidi kumtengenezea maisha bora baadae maskini
 
Back
Top Bottom